Msanii wa muziki wa R&B, Benard Paul ‘Ben Pol’, amedai hali ya
uchumi kwa wasanii ni tete kutokana na kufilisika kwa mapromota wengi
ambao walikuwa wanaandaa show nyingi mikoani.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Moyo Mashine’ ameiambia
Bongo5 kuwa hali hiyo imewafanya wasanii wengi akiwemo yeye kushindwa
kutimiza malengo yao ndani ya mwaka huu.
“Plan zimebadilika sana mwaka huu na plan zimebadilika kwa sababu nyingi
kwanza mfumo mzima wa biashara umebadilika sio kama miaka iliyopita,”
alisema Ben Pol. “Yaani hiki ni kitu ambao wasanii wenzangu
watakubaliana na mimi, mzunguko wa pesa na kazi umeshuka kidogo
ukilinganisha na miaka mingine. Kwahiyo unaweza ukawa na matarajio yako
au mipango ukashindwa kutumiza au ikawa tofauti,”
Aliongeza, “Mapromota wengi wamefilisika hasahasa wale wa mikoani, wengi
hawawezi tena kuandaa show wenyewe, wakiomba sponsorship zinasuasua,
yaani hela hamna, kwa hiyo wanachokifanya sasa hivi ni kuwa partners na
wasanii ili kuandaa show,”
Muimbaji huyo amesitisha kuachia albamu yake mpya ambayo alitangaza kuiachia mwishoni mwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment