Monday, 18 April 2016

Kim Kardashian ameomba Talaka Kwa Kanye West


Ndani ya wiki mbili zijazo,huenda Kim Kardashian akaanza Taratibu za kuomba Talaka kutoka kwa mume wake,Kanye West.

Kama hilo litatimia,basi huenda ukawa mwisho wa ndoa hiyo iliyodumu kwa miaka miwili Sasa,kwa mujibu wa vyombo vya habari marekani.
Inadaiwa kuwa,Kardashian (35) amefikia kiwango cha mwisho cha uvumilivu ndani ya ndoa Hiyo.

Mgogoro wa kifedha na mambo ya familia,ndiyo yanayoelezwa kumchosha kimwana huyo kiasi cha kuamua sasa kuomba talaka ili aanze maisha upya.

Lakini pia wapambe wa karibu wa wapenzi hao wanadai kuwa hakuna amani kati yao na kwa Siku za karibuni wamaekuwa wakitumia muda mwingi kulumbana kuliko kufurahia penzi.

No comments:

Post a Comment