Thursday 14 January 2016


W1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa (kulia), akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya mawasiliano ni Profesa Faustin Kamuzora
W2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa akijisajili katika mfumo wa mahudhurio wa elektoniki (kulia), ni Afisa Utumishi Bi, Elizabeth Maduhu akimwelekeza.
W3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa akifungua mlango kwa kutumia mfumo wa mahudhurio wa elektroniki baada ya kujisajili.
W4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa akisaini kitabu cha mahudhurio baada ya kujisajili katika mfumo wa mahudhurio wa elektroniki katika ofisi za sekta mawasiliano.
W5
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa wa (kwanza kulia), akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya mawasiliano Profesa Faustin Kamuzora (katikati) na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Dakta Maria Sasa
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Prof. Makame Mbarawa amezungumzia umuhimu wa taasisi zote za Serikali kuwa na mfumo wa mahudhurio kwa njia ya kielekroniki electronic attendance registration (EAR).

Akizungumza mara baada ya kujisajili katika ofisi za sekta ya mawasiliano Prof. Mbarawa amesema kwa kuanzia utaratibu huo utaendelezwa katika sekta Uchukuzi na Ujenzi na kisha utafungwa katika taasisi zote za Serikali ili kuhakikisha watumishi wa umma wanafika ofisini kwa wakati na kupunguza utoro.
“Hakikisheni watumishi wote wanatumia mfumo huu wa kielektroniki ili kudhibiti utoro na kuwezesha wafanyakazi kufanyakazi kwa muda unaokubalika kiserikali ”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Aidha Waziri Mbarawa amewataka wafanyakazi wa mapokezi kuacha kuwafungulia wafanyakazi watoro na wanaochelewa kazini kuingia ofisini ili kuwezesha mfumo kutambua watumishi watoro na hivyo kuchukuliwa hatua stahiki.

Amesisitiza kuwa mfumo huo utakapofungwa katika taasisi zote za umma utadhibiti watoro kwa kuwa unaweka kumbukumbu ya muda mtu anaokuwa kazini na hivyo kuwawezesha viongozi kupata taarifa sahihi za mahudhurio
SONY DSCWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboje alipoitembelea taasisi hiyo mapema leo. 
SONY DSCWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Taasisi ya Uongozi alipoitembelea taasisi hiyo mapema leo.  
SONY DSCWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akiwa katika kikao kazi na watumishi wa Taasisi ya Uongozi mapema leo. 
SONY DSC
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (mstari wa mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi ya Uongozi alipoitembelea taasisi hiyo mapema leo.  

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) Ameielekeza Taasisi ya Uongozi kufanya tathmini ya fursa za mafunzo zinazotolewa kwa Watumishi wa Umma kama zinakidhi mahitaji ya nchi.
Waziri Kairuki alisema hayo leo alipokutana na Watumishi wa Taasisi hiyo jijini Dar es salaam.
“Mafunzo yanayohudhuriwa na Watumishi wa Umm kwa mahitaji yetu”elekezaWazirinakuongeza niKairukijambolamsingi alikuainisha
maeneo yanayohitaji kuboreshwa katika eneo la kujenga uwezo ili kufikia malengo.
Waziri Kairuki alisisitiza kuwa tafiti katika maeneo ya utoaji huduma kwa upande wa Sekta ya umma zipewe msukumo na mapungufu yatakayobainika baada ya tafiti kukamilika yaelezwe bayana ili kupata kupata Mrejesho.
Kwa upande wa viongozi wa umma Mhe. Kairuki alisema ni vema wapate mafunzo katika masuala mtambuka ili wafanye kazi kwa taratibu zilizowekwa.
Taasisi ya Uongozi, pamoja na masuala mengine huendesha Programu za mafunzo kutokana na mapungufu yanayoonekena kupitia tafiti mbalimbali zinazofanyika.
Taasisi ya Uongozi ilianzishwa kwa ushirikiano baina ya Serikali za Tanzania na Finland na kutangazwa katika gazeti la serikali la Tarehe 30 Juni, 2010.

No comments:

Post a Comment