Monday 18 January 2016

Z8
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Botswana, Bw. Tshenolo Mabeo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sir Seretse Khama  uliopo  Gaborone Januari 2016. Majaliwa amemwakilisha Rais John Magufuli katika Mkutano wa SADC.
Z9
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mtendaji wa SADC,Dkt, Srergomena Tax mjini Gaborone ambako Mheshimiwa Majaliwa anamwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa SADC 

Z1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa akiweka saini kwenye kitabu cha kumbukumbu mara alipowasili Mkoani Lindi kwa Ziara ya Kukagua miradi inayotekelezwa na Wizara hiyo.Kulia ni ni Bi.Mariam Mtima Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa.
Z2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa akipokea taarifa ya Ujenzi wa barabara ya Mangaka-Mtambaswala (KM 62.7), kutoka kwa Mhandisi Mkazi Anold Msengezi (Katikati) anayesimamia ujenzi wa barabara hiyo.
Z3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo juu ya Ujenzi wa barabara ya Mangaka-Mtambaswala (KM 62.7), ambapo amemtaka Mkandarasi kukamilisha Ujenzi huo kwa wakati na ubora unaokusudiwa.
Z4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia) akipokea taarifa ya Ujenzi wa barabara ya Mangaka –Nakapanya (KM70.5) kutoka kwa Mhandisi mkazi Dkt.Chaurasia inayojengwa na kampuni ya Jiangxi Geo Engineering (Group) Cooperation ya China.
Z5
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na wakazi wa Nakapanya alipopita kukagua bujenzi wa barabara ya Mangaka-Mtambaswala (KM 62.5).
Z6
Sehemu ya barabara ya Mangaka –Mtambaswala (KM 62.5) ambayo Ujenzi wake unaendelea kwa kiwango cha lami.
Z7
Na Mwandishi wetu
Tingatinga likiwa linaendela na kazi za ujenzi barabara ya Mangaka –Mtambaswala (KM 62.5) ambayo Ujenzi wake unaendelea kwa kiwango cha lami.

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewataka makandarasi wanaojenga barabara za Mangaka-Mtambaswala KM 62.7 na Mangaka-Nakapanya Km 70,5 kukamilisha ujenzi huo ifikapo Juni mwaka huu.
  Amewataka makandarasi hao kuongeza Rasilimali watu na vifaa ili ujenzi huo ukamilike kama ilivyopangwa katika mkataba wa ujenzi wake.
  “Hakuna muda utakaoongezwa nataka miradi yote miwili iwe imekamilika ifikapo juni mwaka huu tena iwe kwenye ubora unaowiana na thamani ya fedha,”amesema Waziri Prof. Mbarawa. Barabara hizo ambazo ujenzi wake kwa kiwango cha lami ulianza mwaka 2014 zitafungua fursa za kiuchumi mkoani Mtwara ikiwemo kuiunganisha Tanzania na Msumbiji kwa lami kupitia daraja la umoja lililoko Mtambaswala.
  Akizungumza katika ziara hiyo Meneja wa Wakala wa Barabara TANROADS mkoa wa Mtwara Eng. AISHA SALIM amesema hawata kubali maombi yoyote ya kuongeza muda wa ujenzi wa barabara hizo ambapo ujenzi wa barabara ya Mangaka –Mtambaswala Km 62.7 unatarajiwa kukamilika mwezi Mei na ule wa Mangaka-Nakapanya KM 70.5 ukitarajiwa kukamilika mwezi julai mwaka huu.
  Mapema Prof. Mbarawa alikagua hali ya barabara wilayani Ruangwa,Nachingwea na Masasi na kusisitiza kuwa ujenzi wa barabara na madaraja katika wilaya hizo utaendelea katika kipindi kifupi baada ya Serikali kuanza kutoa fedha kwa miradi inayotumia fedha za Mfuko wa Barabara (RFB).
  Waziri Mbarawa yuko katika ziara ya mikoa ya lindi na mtwara kukagua miradi ya Barabara,Mawasiliano na Bandari ili kuona ufanisi uliopo katika sekta hizo. Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano

No comments:

Post a Comment