Thursday 21 January 2016




 Image result for Muhingo Rweyemamu

Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya Morogoro Ameagiza polisi kuwakamata Wanakijiji wa Kisaki Stesheni Waliohusika na Mapigano kwa kutumia silaha za jadi jana tarehe 20/01/2016 katika Mkutano wa Hadhara uliyolenga kutoa Ufafanuzi wa Mgogoro huo.

Mkuu wa Wilaya Bw.Muhingo Rweyemamu ameyasema hayo leo Alipokuwa Akizunguza kwa njia ya simu Alipohitajika kutoa ufafanuzi kuhusu tukio la uvunjifu wa amani kwa wanajikiji hao waliyokuwa na Mgororo Wa Ardhi unaowahususha Wakulima na Wafugaji.

“Mgogoro huu wa Ardhi umesababishwa na Mwenyekiti wa Kijiji Bw. Ismail N’ganji kwani aligawa ardhi Hiyo ya kijiji Mara Mbili kwa wakulima na wafugaji wakati katika taratibu za kugawa Ardhi ni lazima Wanakijiji Waamue katika kikao cha kijiji, na maombi ya kuomba ardhi ya Kijiji cha Kisaki yalikuwa kati ya Wakulima na Wafugaji ambao kijiji kiliadhimia kuwa ardhi hiyo ipewe wafugaji ambapo Mwenyekiti wa Kijiji Aliamua kugawa Ardhi hiyo kwa Wakulima kinyume na Makubaliano ya Mkutano wa Kijiji na hapo ndipo Chanzo cha Mgogoro huo ulipoanza”, alisema Bw.Rweyemamu.

Mbali na hayo Bw. Rweyemamu alisema mpaka sasa mwenyekiti huyo wa kijiji ameshafukuzwa na uchaguzi Wa Mwenyekiti mwingine unatarajia kufanyika hivi karibuni nakuwataka viongozi wa kijiji kuzingatia sheria Za Ugawaji ardhi na kuacha kukiuka misingi hiyo kwani ndiyo inayosababisha migogoro mingi ya ardhi katika Maeneo mbalimbali.
Akiendelea kuzungumza mkuu huyo 
Wa wilaya alisema Sheria ya Ardhi inaeleza vizuri endapo mtu atahitaji ardhi isiyozidi heka 50 basi ni lazma Awasilishe Maombi hayo kwa Mkuu wa wilaya na Wanakijiji wahusishwe katika kikao cha maamuzi ya kuridhia na kwa Upande wa mtu atakayehitaji Ardhi Zaidi ya heka 50 basi Maombi yatatakiwa kuwasilishwa kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya hiyo alisema Migogoro ya ardhi imekuwa inasababishwa na Viongozi wa kijiji kwa kiasi kikubwa kwani baadhi yao wamekuwa wakiendekeza Rushwa huku wakisababisha uvunjifu wa Amani kwa Wanakijiji hivyo wito wake ni viongozi hao Wazingatie Maadili ya kiutendaji na kuachana na Vitendo vya Rushwa.

No comments:

Post a Comment