Tuesday 5 January 2016

Bomobomoa Yasitishwa Dar


Image result for PICHA ZA BOMOABOMOA DAR

Na Kalonga Kasati
Mahakama Kuu Tanzania Kitengo cha Ardhi inatarajia kutoa Hukumu ya kuiruhusu Serikali kuendesha shughuli ya Bomoa Bomoa kwenye Makazi ya mabondeni au kuizuia kuendesha Shughuli Hiyo Januria 5, Mwaka huu.

Kesi Hiyo ya kupinga kubomolewa kwa Wakazi hao Bila kupatiwa Makazi mengine salama imefunguliwa kwa hati ya Dharura na Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulya chini ya Wakili Wake, Abubakar Salim huku  Serikali ikiendelea na operesheni ya kuweka alama za X kwenye nyumba zaidi ya 3000.

Katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi iliyopo katikati ya Jiji la Dar Es Salaam ambapo Umati wa Wananchi wa Mabondeni kwenye Manispaa ya Kinondoni umekusanyika ili kupata hatma ya Makazi yao.

Katika kesi hiyo kuliibuka mabishano ya kisheria baina ya Wakili wa Upande wa Serikali, Gabriel Maleta anayeiomba Serikali kutupilia mbali maombi hayo ya dharula kutokana na kushindwa kukidhi vigezo ikiwa ni pamoja na hati yake kutobainisha walengwa jambo linalopingwa na Wakili wa Waleta Maombi.

Katika Pingamizi Lake, Wakili Salim amedai kuwa lazima mahakama iwalinde wateja wake kutokana na kukimbilia kwenye sheria ili iwatendee haki.
Jaji Panterine Kente ameahirisha kesi hiyo hadi Januria 5, Mwaka huu saa Tano.

Wakati hayo yakiendelea huko Mahamani zaidi ya Nyumba 3000 jijini Dar Es Salaam zimewekwa Alama za X Tayari kwa kubomolewa.
Ubomozi wa Nyumba hizo Umekuja ikiwa ni Utekelezaji wa Agizo la Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  William Lukuvi la kutaka kuwaondoa wakazi waliovamia Maeneo hatarishi, wazi na mabondeni.

Kufuatia uwekaji wa Alama hizo Fofammedia ikazungumza Na Baadhi ya Waathirika ambapo Wamesema waonyeshwe Maeneo Ambayo wataenda kuishi
 Oparesheni ya Bomoabomoa ilianza Jijini Dar es Salaam Mwishoni mwa mwaka Jana ambapo Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Baraza la Mazingira Tanzania (NEMC).

No comments:

Post a Comment