Saturday 30 January 2016

11
Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakipata maelezo ya Kitaalam kutoka kwa Mshauri Mwelekezi walipotembelea mradi huo kujionea hatua mbalimbali za ujenzi. Wengine ni Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Kilombero.
……………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu Morogoro
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya Amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya “Tanzania Building Works ya Jijini, Dar es Salaam” inayojenga Mradi wa Umwagiliaji Gereza la Kilimo Idete kuukamilisha mradi huo katika muda Walioongezewa ili kuwezesha kuanza kwa shughuli za uzalishaji gerezani hapo.
 
Akizungumza na Wakandarasi wa Kampuni hiyo alipofanya ziara ya kikazi Gereza Idete, Balozi Yahya amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo ni mkombozi kwa Jeshi la Magereza kwani Utawezesha uzalijashi wa chakula cha kutosha cha wafungwa waliopo magerezani pamoja na kuzalisha ziada itakayouzwa kwa Wananchi ili kuongeza Mapato Serikalini.
“Ni matarajio yangu kuwa Mkandarasi wa Mradi huu kwa kushirikiana na Mshauri Mwelekezi na Wadau wa Jeshi la Magereza atakamilisha mradi huu kwa wakati kama alivyotuahidi hivyo kuanza mara moja shughuli za uzalishaji”. Alisisitiza Balozi Yahya.
 
Naye Msimamizi wa mradi huo Mhandisi Lodia Mallion alisema kuwa mradi huo umekamilika kwa asilimia 60 ambapo tayari uchimbaji na ujenzi wa mifereji itakayokuwa ikipitisha maji kwenda mashambani imekwisha kukamilika.
 
“Mito inayotumika kama vyanzo vya maji ni mto Kilombero pamoja na mto Kiwiliwili ambapo Banio linalotunza maji kwa shughuli za umwagiliaji tayari limekamilika”. Alisikika Mhandisi Mallion.
 
Awali Mkuu wa Gereza Idete, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Nsajigwa Mwakenja akiwasilisha taarifa kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Yahya amesema kuwa kazi ya kuandaa mradi huu ilianza rasmi mwaka 2013 ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika Mwaka huu 2016 ambapo gharama za mradi huo zinakadiriwa kufikia kiasi cha Tsh. 2.5 Bilioni
.
Aidha amesema kuwa chakula kitakachopatikana katika mradi huo wa Gereza Idete kitatumika kulisha wafungwa waliopo magerezani na ziada itakayopatikana itauzwa kwa Wananchi hivyo kuongeza pato la Taifa.
 
Gereza la Kilimo Idete lipo Wilayani Kilombero, Mkoani Morogoro linajishughulisha na Kilimo cha Mpunga wa chakula na pia mpunga kwa ajili ya mbegu bora za Kilimo hapa nchimi. Gereza hilo lilianzishwa rasmi mwaka 1983 kwa ajili ya Kilimo cha mazao mbalimbali hususani Kilimo cha mpunga.

Mwonekano Wa Unavyoonekana Katika Lango Kuu La Kuingilia Uwanja Wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Mwonekano katika lango Kuu la Kuingilia katika Uwanja wa mpira wa CCM Kirumba Jijini Mwanza pindi mvua inaponyesha. Ni zaidi ya Usumbufu, kero na Adha kwa wanaoingia na kutoka Uwanjani hapo pindi mvua inaponyesha.
Ni zaidi ya Usumbufumbu kwa mashabiki wa mpira pindi mvua inaponyesha wanapokuwa wakiingia amba kutoka Uwanjani, katika Uwanja wa CM Kirumba Jijini Mwanza kutokana na maji kutuama katika barabara inayoingia na kutoka katika lango Kuu la kuingilia Uwanjani hapo.
Wahusika mlione hili kama changamoto inayopaswa kutafutiwa utatuzi.

No comments:

Post a Comment