Saturday 23 January 2016

 ME2
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii,Bi. Uzeeli Kiangi akisisitiza jambo wakati alipokuwa anamkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja. Generali. Gaudence Milanzi kufungua Mkutano Mkutano wa Kamati ya Uwezeshaji Utalii ( Tourism Facilitation Committee- TFC) uliofanyika leo Mpingo House jijini Dar es Salaam wa kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Utalii nchini.
ME1
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja. Generali. Gaudence Milanzi ( kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Bw. Deogratius Mdamu (kushoto) wakimsikiliza Mjumbe ( hayupo pichani ) wakati wa Mkutano wa Kamati ya Uwezeshaji Utalii ( Tourism Facilitation Committee- TFC) uliofanyika leo Mpingo House jijini Dar es Salaam akiwa anazungumzia changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Utalii nchini na kutoa ushauri ya namna kuuimarisha Utalii wa ndani ambao umekuwa bado ni changamoto kwa wananchi wengi kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini
ME3
 Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Uwezeshaji Utalii ( Tourism Facilitation Committee- TFC) wakiwa wanajadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Utalii nchini kwa kutoa maoni, ushauri na ufumbuzi wa changamoto ikiwa na kuchangia mikakati mbalimbali itakayowezesha kusaidia kuhamasisha Utalii wa ndani.
…………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Wakati nchi nyingi Afrika zikiwa zinafanya jitihada mbalimbali za kuimarisha Utalii wa ndani ambao umekuwa ndo wa uhakika katika kuiingizia nchi mapato hata pale majanga yanapotokea, Nayo Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kuhakikisha kuwa Utalii wa ndani unakua kwa kasi inayotarajiwa.
Baadhi ya Majanga hayo yanayoathiri Sekta ya Utalii ni milipuko ya magonjwa kama Ebola, matukio ya Ugaidi Kenya na kushuka kwa Euro ya Ulaya dhidi ya Dola ya Marekani.
Hivyo Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wadau wa Utalii nchini wamepanga mikakati ya kuhakikisha kuwa Utalii wa ndani unakuwa tegemeo tofauti na sasa ambapo Watalii kutoka nje ndio wamekuwa wamekuwa wakitembelea hifadhi zetu kwa kiasi kikubwa.
Akizungumza kwenye Mkutano wa Kamati ya Uwezeshaji Utalii ijulikanayo kama Tourism Facilitation Committee ( TFC) uliofanyika leo Mpingo House jijini Dar esSalaam , Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili, Meja. Generali. Gaudence Milanzi na Utalii amesema maendeleo ya Utalii yanahitaji sana Utalii wa ndani kuimarika baadala ya kudhani kuwa vivutio vya utalii vilivyopo ni kwa ajili ya wageni kutoka nchi za nje.
Meja. Generali. Milanzi amesema Utalii ni sekta nyeti sana katika kuliingiza Taifa pesa za kigeni lakini hata hivyo ni sekta ambayo imekuwa inaathirika kwa haraka sana pindi majanga yanapotokea nchi jirani hivyo ni lazima jamii ijengewe utamaduni wa kutembelea vivutio vya Utalii ili kuweza kujihakikishia Watalii wa ndani wanakuwa wengi.
Baadhi ya mikakati iliyopendekezwa na Wajumbe wa kamati ya Uwezeshaji Utalii (TFC) ni kuwawezesha maafisa Utalii wa Halmashauri wanatengewa bajeti ya kutosha, wanajengewa uwezo kuhusu ya vivutio vya utalii vilivyopo kwenye maeneo yao pamoja na Idara ya Utalii kufungua ofisi kila kanda ili kuweza kutimiza majukumu yake ipasavyo.
 
Aidha,viwanja vya ndege vilivyopo nchini viimarishwe ikiwa pamoja na nchi kuwa ndege zake kama ilivyo kwa nchi jirani kama Kenya na Rwanda
Awali , Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii,Bi. Uzeeli Kiangi alisema Mkutano wa TFC hutoa fursa za kuziibua na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Utalii hivyo Sekta Binafsi zinawajibu mkubwa wa kuhakikisha changamoto zinazoikabili sekta zinatafutiwa ufumbuzi
Aliongeza kuwa Idara ya Utalii imekuwa ikishiriki katika maonesho mbalimbali ya kitaifa lengo likiwa ni kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya Utalii nchini.
 
Aidha, Prof Wineastor Anderson amesema sekta ya Utalii imekuwa inakua lakini si kwa kiwango cha kuridhisha hivyo jitihada za kutangaza utalii ndani na nje nchi upewe uzito unaostahili kwa kuiwezesha Bodi ya Taifa ya Utalii inatengewa bajeti ya kutosha.
 
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Utalii Tanzania ( TCT) Bw. Richard Rugimbana, amesema Utalii wa ndani ili uweze kukua suala la elimu linahitajika kutolewa ili kuweza kuibadilisha jamii ipende kutembelea vivutio vya Utalii.
 
Naye Kamanda wa Polisi Jk Ndaki anayeshghulikia dawati la Utalii ( Tourism Police Unit) Amewahakikishia usalama wao watalii wa ndani na nje ya nchi kutembelea vivutio vya Utalii bila hofu yoyote kuwa Jeshi la Polisi nchini lipo macho muda wote.

No comments:

Post a Comment