Tuesday 19 January 2016

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe. Philip Mangula (kulia) akizungumza na Wabunge wa CCM kwenye semina Maalum ya Wabunge Wote wa CCM inayofanyika kwenye Ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, Wengine pichani ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) na Katibu wa NEC Itikadi Na Uenezi Ndugu Nape Nnauye (kushoto). Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa Na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Ndugu Nape Nnauye (kulia) Akizungumza Na Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mkoani Mwanza Mhe. Shanif Mansoor Muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Wabunge wa CCM kwenye Ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya Dk. Mary Mwanjelwa (kushoto) Akizungumza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia Ni Mbunge wa viti maalum Mhe. Annastazia Wambura muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha wabunge wa CCM mjini Dodoma.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana Na Wabunge wa CCM kabla ya kuanza kwa kikao cha Wabunge Hao kwenye ukumbi Wa NEC mjini Dodoma.
vpl15
Ligi Kuu ya Vodacom Mzunguko wa 15 Unatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa Michezo Mitano, na Alhamisi kwa Michezo mitatu kwa kila Timu kusaka pointi tatu muhimu katika Mzunguko huo.
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Maafande wa JKT Ruvu watawakaribisha Simba SC, Ndanda FC watakua wenyeji wa Mbeya City kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Tanzania Prisons Watakua wenyeji wa Coastal Union katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Stand United watacheza dhidi ya Toto Africans kwenye uwanja wa Kambarage, huku Mgambo Shooting Wakiwakaribisha Azam FC kwenye uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Alhamisi ligi hiyo itaendelea kwa michezo mitatu, Mwadui FC watawakaribisha Kagera Sugar katika Uwanja wa Mwadui, African Sports watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar uwanja wa Mkwakwani jijini Tnaga, huku Young Africans Wakiwakaribisha Majimaji FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

sheikhmalinzi
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Asia (AFC), na Makamu wa Rais wa FIFA, Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa leo ametembelea wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Ambapo alifanya mazungmzo Mafupi na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel.
Katika mazugmzo hayo, Sheikh Salman Ameielezea Serikali ya Tanzania nia ya FIFA kuendelea  kushirikiana na Serikali na TFF katika kuendeleza programu Mbalibali za maendeleo ya mpira hasa wa vijana na wanawake.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa Elisante  ameihakikishia FIFA kuwa nia ya Serikali ni kuona mpira unakua nchini na Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa TFF na FIFA ili kufikia Azama hiyo.
Aidha pia Ametoa wito kwa AFC kusaidiana na TFF katika masuala ya exchange programmes ili Vijana wetu wapate Uzoefu wa nje.
Sheikh Salman na ujumbe wake walitembelea ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Wakiwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi, ambapo walikutana na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na kujionea shughuli Mbalimbali Zinazofanya na shirikisho, ikiwemo Uwanja wa Karume, na Hostel zilizopo Karume.
Kiongozi huyo wa AFC, Aliwasali nchini Jana Mchana kwa Matembezi ya Siku Mbili chini ya Mwenyeji wake Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Anatarajiwa kuondoka nchini kesho.
Rais wa Chama Cha Wafamasia Tanzania (PST) Bi. Elizabeth Shekalaghe akitoa maelezo kuhusu wiki ya Famasi Taifa- 2012
Na. Kalonga Kasati

WANANCHI Wameshauriwa kununua Dawa za kutibu magonjwa Mbalimbali wanazoandikiwa na Madakatari  kwenye Maduka ya dawa yenye Mfamasia mwenye Elimu ya shahada ili kulinda  Afya zao kwa kupata dawa sahihi.

Kauli hiyo imetolewa Jana Jijini Dar es salaam na Msajili wa Baraza la Famasi Tanzania, Elizabeth Shekalaghe  Wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Mara Baada ya kufanyika kwa Semina ya kutoa vyeti vya Usajili wa Wafamasia wapya iliyoambatana na shughuli Mbalimbali ikiwemo Nadhiri ya kiapo cha uaminifu kwa Wafamasia ambao Walipewa kitabu cha Miiko ya Taaluma  yao.

Akizungumza wakati wa Semina hiyo Msajili huyo alipiga marufuku Tabia ya Baadhi ya Wafamasia kutundika vyeti vya

Taaluma zao kwenye Maduka ya Dawa kwa lengo la kuonyesha   Uhalali wa kutoa Huduma Wakati Wao wenyewe Hawapo  katika famasia husika.

Aidha, Bi. Shekalaghe  alipiga marufuku  Dawa zenye Nembo ya Serikali kuuzwa kwenye Maduka ya Dawa yasiyomilikiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD), kwani kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na kuongeza kuwa mfamasia  yeyote atakayekutwa na dawa zenye nembo Serikali katika Duka analolisimamia, yeye pamoja na mmiliki watachukuliwa hatua za kisheria.

“Ni Marufuku kwa Dawa zenye nembo ya Serikali kuuzwa katika duka la dawa lisilomikiwa na Bohari Kuu ya Dawa(MSD).Mfamasia  ambaye duka analolisimamia litakutwa na dawa zenye Nembo ye Serikali, yeye pamoja na Mmiliki wake watachukuliwa hatua kali za kisheria,” alisisitiza Elizabeth.

Msajili huyo alisema  Jamii inapaswa kuwatambua watu wanaotoa huduma za dawa, ambao wapo Wenye Elimu ya Taaluma hiyo kuanzia ngazi ya Stashahada ambao huitwa Mafundi Dawa Sanifu Na Wale  Wenye Elimu ya Cheti cha Mwaka  Mmoja na wale wenye elimu ya program Maalum wanaoitwa watoa dawa.

Alisisitiza kuwa jamii inapaswa kuwa na uelewa na kutofautisha kati ya duka la dawa,ambalo lazima liwe na Mfamasia na duka la dawa muhimu ambalo huwa  na watoa dawa. Aidha aliwataka wafamasia hao kukubali kwenda kufanya kazi mikoani ili kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata huduma stahiki za.

“ Kukutana kwetu  hapa kuna umuhimu  mkubwa ikizingatiwa kuwa sasa usimamizi wa utoaji wa huduma za dawa na majengo unalegalega,Tukiweza kuboresha utendaji wetu katika taaluma hii hususan usimamizi wa sehemu za kutolea huduma za dawa tutarudisha hadhi ya taaluma na kulinda afya ya jamii kwa kuwa na matumizi sahihi ya dawa,”alisisitiza Elizabeth.

Aliongeza kuwa Ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko,kesi na migongano kati ya wafamasia na waajiri wao kutokana na kutoa huduma zisizokidhi viwango huku wengine wakifikishwa mahakamani kwa kutuhumiwa kuiba dawa.

“Yote  haya yanaonesha kwamba kuna tatizo na maadili na miiko ya kitaaluma kutofuatwa. Baraza la Famasi kama chombo cha Serikali haliwezi kubaki nyuma kama kisiwa katika kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano.Ni vema tukakumbuka kwamba hivi sasa tunatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sera ya Serikali iliyoko madarakani kwa kauli mbiu ya HAPAKAZI TU,ambayo sisi sote tunapaswa kuielewa,kuitafsiri na kuisimamia katika namna ambayo itaonesha mabadiliko makubwa ambayo ndio lengo letu kama wataalam”

Aliwataka wafamasia hao kutii sheria bila shuruti na kuzisoma na kuzielewa sheria na kanuni zilizopo.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa baraza hilo Bw. Lagu Mhangwa aliwataka wafamasia hao kuwa Na Tabia kujiendeleza kielimu ili kuendana na mabadiliko ya taaluma ya dawa yanayotokea na kuandika miradi mbalimbali ambayo itakayowasaidia kubadilisha taaluma ya fani hiyo nchini.

No comments:

Post a Comment