Monday 18 January 2016

MKW1
Katika Maeneo ya Mkwajuni Kinondoni Baadhi ya Wananchi Wamefunga Barabara Wanachoma Matairi kwa kile wanachodai kupinga Bomoa Bomoa Askari wako eneo la tukio Wakijaribu kuwazuia kufanya Matukio Hayo na Hakuna Magari Yanayoweza kupita Eneo hilo Kutokana na Vurugu Zilizoababisha  kufungwa kwa Barabara Hiyo ya kutoka Moroco kwenda Magomeni.
MKW2 MKW3

msangi

MTU MMOJA MKAZI WA MADIBIRA WILAYANI MBARALI MKOA WA MBEYA AITWAYE KULWA BIDA [38] ALIUAWA NA WANANCHI WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KUPIGWA MAWE NA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE BAADA YA KUTEREMSHWA KWENYE GARI LA LESAME KWA TUHUMA ZA KUMTOROSHA  MTOTO AITWAYE KANG’WA MASUNGA [13] MKAZI WA MADIBIRA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 17.01.2016 MAJIRA YA SAA 20:16 USIKU HUKO BARABARA YA MADIBIRA, KUELEKEA MAFINGA, KATA YA MADIBIRA, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA NI BABA MKUBWA WA MTOTO HUYO NA ALIKUWA AKIMTOROSHA KWA LENGO LA KWENDA KUMLEA. AIDHA KUTOKANA NA TUKIO HILO, WATUHUMIWA WAWILI WAMEKAMATWA KUHUSIKA NA TUKIO HILO AMBAO NI 1. MAHELA MAGO [30] MKAZI WA IKOGA 2. MASAYA MADENI [36] MKAZI WA NYAMAKUYU AMBAYE NI MLEZI WA MTOTO HUYO.
JUHUDI ZA KUWATAFUTA WATUHUMIWA WENGINE ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUJEWA NA UPELELEZI UNAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI EMANUEL G.LUKULA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA VITENDO VYA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI.
TAARIFA ZA MSAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, MTU MMOJA MKAZI WA MKANGE WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA AITWAYE TUSAJIGWE MSHANE [45] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI @ GONGO UJAZO WA LITA 10.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 17.01.2016 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MKANGE, KIJIJI CHA ISANGAWANA, KATA YA MTWIGA, TARAFA YA KIPAMBAWE, WILAYA YA CHUNYA NA MKOA WA MBEYA.
KATIKA MSAKO WA PILI, MTU MMOJA MKAZI WA MKANGE WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA AITWAYE JAMES AYUBU [38] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI @ GONGO UJAZO WA LITA 01.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 17.01.2016 MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MKANGE, KIJIJI CHA ISANGAWANA, KATA YA MTWIGA, TARAFA YA KIPAMBAWE, WILAYA YA CHUNYA NA MKOA WA MBEYA.
WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA TU BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA.
Imesainiwa na
[EMANUEL G.LUKULA – ACP]
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)Mhandisi Suleiman Said afariki dunia, Kuzikwa makaburi ya kisutu leo

SUL1
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman Said amefariki dunia mapema leo asubuhi akiwa katika mazoezi ya kuogelea,taarifa zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo Bwa.Suleiman alikimbizwa hospitali ya Agakhan kwa matibabu,na baadae ikaelezwa kuwa amekwishafariki na kuwa mazishi yanatarajiwa kufanyika leo. Marehemu alipata kuwa Katibu mkuu wa Simba.

Taarifa zaidi zinasema Marehemu Mr Sukeiman aliamka asubuhi akamwambia mke wake hajiskii vizuri, lakini alienda baharini kuogelea kama kawaida yake. Walikuwa wawili na mwenzie, wakaenda mbali sana wakati wa kirudi aliishiwa nguvu, alijitahidi akafika nchi kavu akiwa hoi kabisa amekunywa maji wengi na akawa anatokwa na mapovu mdomoni. Alifariki njiani akipelekwa hospitali. Msiba upo upanga nyuma ya jeshi (Ngome) saa hii maiti imefuatwa wanakuja kuaga  hapa nyumbani, mwili utarudi msikitini saa tisa kisha kuzika makaburi ya Kisutu nyuma ya chuo cha CBE. Apumzike kwa Amani.

Kinana alitakia heri Tamasha la Pasaka 2016

Abdulrahman_KinanaNa Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amelitakia heri Tamasha la Pasaka la mwaka huu linaloandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions ambalo litafanyika baadaye mwaka huu.
Akizungumza mwishoni mwa wiki, ofisini kwake, Lumumba jijini Dar es Salaam, Kinana analitakia heri na fanaka tamasha hilo na kumuomba Mungu aendelee kubariki utulivu na mshikamano kwa Watanzania wote.
Kinana alisema Tamasha la Pasaka lengo lake ni ujenzi wa Taifa letu na kudumisha amani na utulivu tulionao sambamba na jukumu kubwa la kupiga vita umasikini na kuboresha maisha ya Watanzania na kufikia kiwango cha juu cha maendeleo.
Kinana alisema Watanzania tuna wajibu  wa kudumisha mshikamano na upendo miongoni mwetu na tuendelee kusaidiana katika kila hali.
“Tamasha la Pasaka mwaka huu liwe ni muongozo wa kudumisha mshikamano na upendo miongoni mwetu ili tuendelee kusaidiana katika kila hali,” alisema Kinana.
Katibu huyo alisema Watanzania tunatakiwa kuzingatia hayo ili sote kuwa pamoja ili tupige hatua stahili na kuondokana na umasikini uliokithiri.

No comments:

Post a Comment