Monday 18 January 2016

TFDA

MAMLAKA ya Chakula na dawa TFDA, imeaanza kutoa Elimu ya kula chakula salama kwenye shule Mbalimbali za mkoa wa Arusha ili kuwezesha wanafunzi na Jamii kuepukana na Magonjwa ya maambukizi yanayosababisha vifo na Madhara Mengine ya kiafya.
Meneja Wa Mamlaka ya Chakula na dawa TFDA, kanda ya kaskazini, Damas Matiku, Amesema Elimu hiyo inayotolewa ikiwa ni Sehemu ya Maadhimisho ya siku ya Chakula Dunani Ambayo imeanza Januari 19 na kilele ni Januari 25 .
Matiko ,alisema Maadhimisho Hayo Yanawalenga  zaidi Wanafunzi ambao ni Waathirika Wakubwa kutokana na kutokuzingatia kanuni za chakula salama hususani kuangalia muda wa Vyakula Wanavyokula kama matumizi yake yamekwisha mda wake.
Akielimisha Wanafunzi wa shule za Msingi Ekenywa na Kiranyi, kwa pamoja wilayani Arumeru, Mkaguzi wa chakula na Dawa wa TFDA, Barnabas Jacobo , amesema lengo la kutoa Elimu hiyo ni kulinda afya za Walaji hasa Wanafunzi ambao  ndio Waathirika Wakubwa wa Chakula salama.
Amewaambia Wanafunzi hao kuwa wanapaswa kuishi kwa kuzingatia kanuni za chakula ili Waepuke kupata Maambukizi ya magonjwa mbalimba kama vile  kuumwa na tumbo, kuhara, kuhara Damu, kutapika, kuishiwa nguvu mwilini, homa ya matumbo, kichefu chefu,homa ya Bonde la ufa, kifua kikuu, kimeta, minyoo ,kipindu pindu .
Jacobo,Ameongeza kuwa kupitia maadhimisho hayo wanafunzi na jamii yakiwemo makundi Ya wafanyabiashara ya Matunda na mboga mboga, pamoja na mama lishe watapatiwa elimu Hiyo ili waweze kuzingatia kanuni sita za chakula na hivyo kuepuka kupata magonjwa ya kuambukiza.
Kwa upande Wao Walimu wa Shule za Msingi Kirenyi na Enyuata, wameupongeza mpango huo Wa TFDA, wa kutoa elimu hiyo Muhimu na Utaongeza Uelewa zaidi kwa Wanafunzi katika kuzingatia kanuni za Chakula Salama.
Mkuu wa shule ya msingi Kiranyi Eliafile Issangya, amesema mpango huo utasaidia kupunguza Magonjwa ya matumbo kwa wanafunzi na walimu watatilia mkazo zaidi kufundisha  uzingatiaji wa kanuni za chakula .
Kwa upande wake mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi Enyuata mwalimu, Simon Laizer , Alisema Elimu hiyo itasaidia kuelimisha na kuzingatia uaandaaji wa vyakula salama hivyo kuondoa magonjwa ya kuambukiza kwa wanafunzi . 
Akizungumza Shuleni hapo kuhusu utekelezaji wa mpango huo Afisa afya wa kata ya Kiranyi, Joseph Mpelumbe, amesema kuwa matumizi ya vyoo katika kata hiyo na maeneo mengine ya wafugaji sio rafiki na bado ni ya kiwango cha chini.
Alisema ofisi ya Afya ya kata imejipanga kuanza kutumia sheria ili kuhakikisha kila mmoja Anakuwa na choo na anakitumia hivyo kupunguza uchafuzi wa mazingira unaotokana na kujisaidia hovyo na matokeo yake ni kueneza magonjwa.

No comments:

Post a Comment