Tuesday 26 January 2016

TRA yawaomba wananchi kutoa Ushirikiano

indexNa Kalonga Kasati
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa Taarifa za Maafisa wanaofanya kazi kinyume na maadili.
Akiongea na mwandishi wa habari Wa Fofammedia hii leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo amesema kuwa TRA ina Idara Maalumu ijulikanayo kama Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA ambayo inashughulika na kufuatilia Maadili ya watumishi wa sekta hiyo nchi nzima.
“Tunawaomba wananchi kushirikiana na Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA kwa kuwapa Taarifa Juu ya Maafisa wa TRA wanaokwenda kinyume na Maadili ya Utumishi wa Umma,”alisema Kayombo.
Mkurugenzi Kayombo ameongeza kuwa wananchi wanaweza kutoa Taarifa kwa kupiga simu kwa namba 0689122515 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwa simu namba 0689122516  na kuwahakikishia kuwa taarifa zao zitakua zimefika sehemu husika na zitafanyiwa kazi.
Aidha Kayombo amependa kuwatoa wasiwasi wananchi kuwa namba hizo ni za siri na hakuna Mwananchi atakayepata tatizo lolote kwa kutoa taarifa za maafisa wasio na maadili.
TRA kupitia Idara yake ya Mambo ya Ndani imepokea malalamiko mengi kutoka kwa Wananchi juu ya watumishi wa TRA wanaoenda kinyume na maadili, wameyafanyia Uchunguzi na Baadhi ya Watumishi wamefukuzwa na wengine kupewa adhabu kali.

Madaktari  Bingwa Kutoka  China Wakishirikiana NaMadaktari Wa Zanzibar Watoa Huduma Za MatibabuKwa Wananchi Wa Kijiji Cha Matemwe Unguja

S2Dokta Abdull Maulid Abdull akimpima Miwani ya kuonea Mwananchi Chale Muumin Fumu mkaazi wa Kijiji cha Matemwe Tunda ngaa katika matibabu yalio fanyika skuli ya matemwe mkoa wa Kaskazini unguja.
S3Dokta Rajab Mohd Haj akimkagua Jicho Mzee Muhidin M Ali Mkaazi wa Kijiji cha Matemwe katika matibabu yaliofanyika Skuli ya Matemwe Mkoa wa Kaskskazini Unguja.
S4Dokta Fei Jie kutoka China akimpima Masikio Bi Fatma Khamis Jaku mkaazi wa Kijiji cha Matemwe  Mfuruni katika matibabu yalio fanyika Skuli ya Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja.
S5Mtoto Iddi Khamis Juma akipatiwa huduma ya kupimwa uzito.
S6Daktari Bingwa kutoka China Yun Lai Gao kushoto na  Mwanafunzi kutoka Zanzibar School of Health Machano M Ali kwa pamoja wakipata maelezo kutoka kwa Mgonjwa anaesumbuliwa na maradhi ya Ganzi Haji Ali Mcha kabla ya kumtibu huko Skuli ya Matemwe.
S7Dokta Yu Lu akimgonga ngumi Mgonjwa anaesumbuliwa na maradhi ya Mgongo Mkadam Vuai kwaajili ya kumpatia matibabu ambayo yamekua yakimsumbua kwa muda mrefu.
S1Mwandishi wa habari wa Star TV Abdalla Pandu akimuhoji Mwanchi wa Kijiji cha Matemwe Mbupurini Chida Pili Khamis Juu ya Huduma za Afya zilizowafikia katika kijiji chao cha Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja.

No comments:

Post a Comment