Friday 8 January 2016


 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Balonzi wa Uturuki Nchini Tanzania, Yasemin Eralp katika picha ya pamoja.  Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo katikati mbele akiwa katika kikao hicho.

Na Kalonga kasati
Serikali ya Uturuki imeomba kuwekeza katika Sekta ya Nishati Nchini Hususani Umeme ili kusaidia Upatikanaji wa Umeme wa kutosha na wa Uhakika.

Ombi hilo linafuatia kikao baina ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Huku pia Balozi huyo Akigusia uwekezaji katika sekta za Kilimo na Utalii.


Vilevile, Balozi Eralp Aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwakaribisha kuwekeza katika Sekta ya Umeme na pia Alimshukuru Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kwa kuwa Muwazi na kuufahamisha Ujumbe huo kuhusu Fursa za Uwekezaji Zilizopo Nchini kupitia Sekta za Nishati na Madini.


Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Alitumia Nafasi hiyo kumweleza Balozi Eralp na ujumbe Wake kuhusu fursa za uwekezaji kupitia vyanzo mbalimbali vya Nishati ikiwemo Nishati Jadidifu, Gesi Asilia, Makaa ya Mawe ili kuzalisha umeme ikiwemo pia sekta ya Madini.


Prof. Muhongo pia Alieleza kuhusu Uwekezaji katika Sekta ndogo Za Mafuta na Gesi Hususani katika Kitalu kilichopo Upande wa Kusini Mashariki mpakani Mwa Tanzania na Msumbiji, Eneo Ambalo Profesa Muhongo alieleza kuwa, Serikali inahitaji Mwekezaji mbia.


“Kipo Kitalu upande wa Kusini Mashariki mwa Tanzania na Msumbiji Ambacho Serikali ya Tanzania inahitaji Mwekezaji Mbia. Mnaweza kushirikiana na Shirika letu la Maendeleo ya Petroli Tanzania. (TPDC),” Alisisitiza Profesa Muhongo.


Pia, Profesa Muhongo Alimweleza kuhusu Maeneo Mengine Yanayohitaji Uwekezaji   kuwa ni Malagarasi, Kakono na Ruhuji. “Lakini pia Mnakaribishwa kuwekeza katika Madini, Tunayo Madini Ya Aina nyingi Nchini ikiwemo Dhahabu,” alisema Profesa Muhongo.


Vilevile, Waziri Muhongo alimweleza Balozi Eralp kuhusu kuisaidia Tanzania katika Suala la Elimu, Hususani Ufadhili wa Masomo katika Ngazi za Uzamivu na Uzamili katika Upande wa Masomo ya Jiolojia, Mafuta, Gesi na Maeneo Mengine.

Akijibu Ombi hilo, Balozi Alimweleza kuwa, “Uwezekano wa Ufadhili wa Masomo Hayo Upo na Mara Nyingi Taratibu za kutuma Maombi Huanzia Mwezi Aprili’,” Alisema Balozi Eralp.

No comments:

Post a Comment