Saturday 16 January 2016

 
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Goodbless Lema Akizungumza katika hafla hiyo.
Na Mwandishi wetu

Halmashauri ya Jiji la Arusha imesaini makubaliano na kampuni ya Bondeni Seeds Limited kupima eneo linalomilikiwa na kampuni hiyo lenye ukubwa wa Hekari 750 ili liwe sehemu ya Master Plan ya  Jiji .

Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro amesema wameshawishika kuingia makubaliano hayo na mwekezaji huyo ili kuwezesha wananchi kuishi kwenye maeneo yaliyopimwa yanayoendana na hadhi ya Jiji na kulipatia mapato yanayotokana naupimaji huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji,Juma Idd amesema Wamekubaliana na mwenye eneo hilo kulipanga na kuliendeleza kama sheria ya makazi inavyotaka.
“Hatutaweza kuendelea na makazi ambayo hayajapimwa kama Unga Limited ,Ngarenaro na mengine ,Arusha ni eneo lenye umuhimu wake katika sekta ya Utalii,madini na ukizingatia hapa ndio Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) na taasisi za kimataifa.
Amesema baada ya kusaini makubaliano utekelezaji Unaanza mara moja ili kufikia malengo ya kuweka mji uliopangika.
Mbunge wa Arusha Mjini,Goodbless Lema amewataka Wananchi wenye Maeneo makubwa kushirikiana na uongozi wa Jiji ili maeneo yao yapimwe kuepusha makazi holela na kuwataka waliojenga maeneo ya mabondeni na kwenye vyanzo vya maji kubomoa nyumba zao.

No comments:

Post a Comment