Wednesday 20 January 2016



New Picture555KUHUSU MAELEZO YA WAZIRI WA AFYA ALIYOYATOA TAREHE 15/01/2016, JUU YA TIBA ASILI NA
TIBA MBADALA.
Ndugu waandishi wa Habari na ndugu wananchi,
shirikisho la vyama vya Tiba Asili Tanzania (shivyatiata) ni chombo
kinachosimamia vyama vyote vya Tiba Asili hapa Nchini pamoja na Waganga wote wa
Tiba Asili na pia ndiyo msemaji wao kwa Serikali, Mashirika ya Kitaifa na
Kimataifa na kuhakikisha chombo hiki kinasimamia na kulinda maslahi yote ya Waganga wa Tiba Asili hapa nchini
Hivyo basi ,kutokana na maelezo yaliyotolewa na Waziri mwenye dhamana na mambo ya Afya mnamo hiyo tarehe
15/01/2016 shirikisho kwa kutambua dhamana tuliyonayo mbele ya Umma wa Waganga
tunapenda kuwasilisha tamko letu kwenu nyinyi waandishi wa Habari na wanchi kwa ujumla ili muweze kuelewa yanayoendelea
katika Tiba Asili hapa nchini.
Ndugu waandishi wa Habari, kwanza mtakumbuka kuwa mnamo tarehe 14/12/2015 Naibu waziri wa Afya maendeleo ya
Jamii, jinsia, wazee na watoto Mhe. Dkt HAMISI KIGWANGALA (MB) alifanya ziara
katika kituo cha Tiba Mbadala cha Tabibu anayejulikana kwa jina la Dr MWAKA.
Baada ya ziara hiyo mengi yalizungumzwa na hata tamko la Wizara lililotolewa
terehe 24/12/2015 lililohusu Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa upande mmoja nalo
lilichangia kuwepo kwa malumbano ya hapa na pale kutoka kwa watoa huduma wa
Tiba Asili na Tiba Mbadala, na wengine wakafikia hatua ya kupinga agizo hilo na kuitisha mgomo.
Ndugu waandishi wa Habari tunapenda mfahamu kuwa Wizara ya Afya katika kufikia kutoa Tamko hilo la tarehe
24/12/2015 hawakushirikisha chombo chenye dhamana ya waganga ambacho ni shirikisho hili la vyama vya Tiba Asili Tanzania, Lakini kwa kutambua dhamana tuliyonayo kwa waganga wote wa Tiba Asili na kwa kutambua kuwa popote panapokuwa na mgogoro basi njia sahihi ni kukaa
mezani kujadiliana ili hatimaye amani ipatikane.
Hivyo sisi Shirikisho tuliomba kikao na Mh. Waziri wa Afya ambacho kilifanyika tarehe 28/12/2015 na ambacho
Kilionesha nuru ya kufikia maelewano, Na kwa kuwa siku hiyo tarehe 28/12/2015 Waziri wa Afya Mhe. UMMY
MWALIMU alitamka mbele ya vyombo vya habari kuwa yupo tayari kukaa kujadiliana
na yeyote Yule ambaye amekwazwa na agizo la Wizara.
Hivyo sisi shirikisho tuliweza kukaa na wadau wa Tiba Asili na Tiba Mbadala ambao kimsingi Ndiyo haswa walikwazika na agizo hilo la Wizara na hatimaye tarehe 31/12/2015 tulifanya kikao cha pamoja kati ya wadau hao, shirikisho, na Wizara ya Afya tukiongozwa na
Uenyekiti wa Mhe. UMMY MWALIMU (MB) ambaye ndiye waziri mwenye dhamana na mambo ya Afya .
Ndugu waandishi wa Habari napenda ifahamike kuwa kikao hicho cha tarehe 31/12/2015 tulikubaliana kuwa wale wote
wanaopeleka matangazo yao na vipindi kwenye Baraza kwa ajili ya kuhakikiwa basi
Baraza liwaruhusu kuendelea na program yao hiyo na uhakiki wa Baraza usizidi siku tatu (3) kwa ujumla makubaliano yote ilikuwa ni utekelezaji wa sheria namba 23 ya  Tiba Asili na Tiba Mbadala ya mwaka 2002 na kanuni zake na pia sheria nyinginezo za nchi na pia utekelezaji huu Uwe wa pande zote, na mwisho Mhe Waziri alituhaidi kuwa tamko lingine la Serikali litatolewa tukiwa wote.

No comments:

Post a Comment