Wednesday 13 January 2016

January 13,2016 Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza Unawakutanisha Watanzania katika Uwanja wa Furahisha Uliopo katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza kwa ajili Ya Maombi ya rasmi ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli Pamoja na Wasaidizi wake ili kuliongoza Taifa vema.
 
Pia Maombi hayo ni mahususi kwa ajili ya kuliombea Taifa kwa ajili ya kupata baraka mbalimbali. Kuanzia majira ya saa Saba Wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wameanza kujongea kwa Ajili ya kujumuika pamoja katika maombi hayo ambayo yatafikia tamati jioni.
 
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo huku wageni mbalimbali wakiwemo Viongozi Wa Dini pamoja na waimbaji nyimbo za injili wakihudhuria katika maombi hayo.

Serikali kuendelea kudumisha ushirikiano na Iran

na1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akikabidhiwa zawadi ya Kitabu cha Mashairi ya Iran na Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Kituo cha Utamaduni wa Iran  hapa nchini Bw. Ali Bagheri alipomtembelea ofisni kwake leo jijini Dar es Salaam.
na2
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akizungumza na Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Kituo cha Utamaduni wa Iran  hapa Nchini Bw. Ali Bagheri alipomtembelea ofisni kwake leo jijini Dar es Salaam.
na3
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akifurahia jambo na Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Kituo cha Utamaduni wa Iran  hapa nchini Bw. Ali Bagheri alipomtembelea ofisni kwake leo jijini Dar es Salaam.

MBUNGE NASSARI ATEMBELEA KARAKANA YA VIFAA TIBA KATIKA MJI GUANGZHOU NCHII CHINA

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akiwa katika moja ya karakana ya kutengeneza Vifaa Tiba katika mji wa Guangzhou nchini China.
Mheshimiwa Nassari akifanya mazungumzo na Wahusika wa karakana hiyo kuona namna ya kuapata Vifaa hivyo kwa Ajili ya kusidia katika Hosptali ya Wilaya ya Arumeru na vituo vya afya.
Mh Nassari akiwa amelala kwenye moja ya vitanda vya wagonjwa alivyokuta katika karakana hiyo.
Mh ,Nassari akipita katika karakana hiyo

No comments:

Post a Comment