Wednesday 22 February 2017

Zidane amkingia kifua Ronaldo

Madrid, Hispania. Zinedine Zidane amesema Cristiano Ronaldo anapenda kucheza kama winga hali itakayomsaidia nyota huyo wa Real Madrid kurejea kati uwezo wake wa kufunga.
Ronaldo hajafunga bao lolote katika mechi mbili zilizopita, ukiwamo ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Napoli katika Ligi ya Mabingwa na ushindi wa 2-0 dhidi ya Espanyol katika LaLiga.
Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari kabla ya safari yake ya Valencia katika mchezo wa ligi leo, kocha huyo wa Madrid alijibu swali kuhusu majukumu ya Ronaldo na mchango wake katika timu.  

"Wakati wote anacheza akiwa anatokea pembeni," alisema Zidane.
"Hiyo ndiyo nafasi yake. Nina uhakika atafunga mabao. Ni mchezaji anayeweza kucheza nafasi nyingi, lakini anapenda kucheza winga. Huko ndiko alipofunga mabao 300, 400?," aliongeza.

No comments:

Post a Comment