Tuesday 21 February 2017

DC Ally Hapi amempa siku saba ofisa elimu wa wilaya ya Kinondoni

. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amempa siku saba  ofisa elimu wa wilaya hiyo  Fatma Mwiru  kuhakikisha idadi ya walimu katika Shule ya Msingi Kiumbageni iliyopo Kata ya Mbweni inaongezeka.
Ametoa amri hiyo leo Jumanne asubuhi kufuatia wanafunzi wa darasa la kwanza 162 kulazimika  kusoma kwenye darasa moja kwa sababu darasa lingine halina mwalimu.

Amesema haamini kama mrundikano huo wa wanafunzi katika darasa moja unatokea kwenye wilaya yake yenye walimu wa kutosha.
Amefafanua kuwa wilaya hiyo katika baadhi ya shule kuna walimu hawana cha kufanya kutokana na kuwa wengi, hivyo wapunguzwe 

No comments:

Post a Comment