Monday 20 February 2017

RT yakamilisha maandalizi hatua ya kwanza Mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika ‘World Cross Country’

 
besu
SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limekamilisha hatua ya kwanza na ya muhimu ya maandalizi ya kuelekea Mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika ‘World Cross Country’ zitakazofanyika Kampala Uganda Machi 26, Mwaka huu.
 
Jumamosi, Februari 18 RT iliendesha Mashindano ya Taifa ya Mbio za Nyika katika Viwanja vya Gofu mjini Moshi mkoani Kilimanjaro na kushirikisha mikoa zaidi ya 11 Tanzania Bara na Visiwani, ambapo wakongwe wengi wa riadha wamekiri kwamba mwamko waliouona juzi haujatokea tangu mwaka 1991 kwenye mashindano yaliyofanyika Arusha eneo la Mushono.
 
Mwaka huo wa 1991, ndiyo mwaka ambao mtanzania pekee Andrew Sambu alishinda mashindano ya Junior ya Dunia Antwerp Belgium, kwa mfano huo sisi Shirikisho la Riadha Tanzania tuna imani kubwa na timu iliyochaguliwa mwaka huu, tunakwenda Uganda kifua mbele, hatuogopi chochote, mataifa mengine nayo yanafahamu kwamba watanzania wameamua safari hii.
 
Kwa vile wengi wenu mlikuwa kwenye tukio juzi, au mathalan habari zote mnazo; napenda sasa nitangaze majina ya wanariadha waliochaguliwa kwenda kusaka medali Uganda na kupeperusha vyema bendera yetu.
Waliochaguliwa kwenye timu ya Taifa kwenda Kampala ni wafuatao:
 
Wanaume Senior 10KM;
1)      Emmanuel Giniki – Manyara
2)      Basil John – CCP / Kilimanjaro
3)      Gabriel Geay – JKT / Arusha
4)      Fabian Joseph – Arusha
5)      Wilbado Peter – CCP / Kilimanjaro
6)      Josephat Joshua – CCP / Kilimanjaro
 
Wanawake Senior 10KM;
1)      Magdalena Shauri – JKT / Arusha
2)      Angelina Tsere – JKT / Arusha
3)      Failuna Abdi – Arusha
4)      Sara Ramadhani – Arusha
5)      Jackline Sakilu – JWTZ / Arusha
6)      Siata Kalinga – JWTZ / Arusha
 
Wanaume Junior 8KM;
 
1)      Francis Dambel – Manyara
2)      Yohana Elisante – JKT / Arusha
3)      Ramadhani Juma – Arusha
4)      Elisha Wema – Arusha
5)      Anthony Wema – Arusha
6)       Joshua Elisante – Arusha
 
Wanawake Junior 6KM;
1)      Cecilia Ginoka – JKT / Arusha
2)      Maicelina Issa – JKT / Arusha
3)      Asha Salum – JKT / Arusha
4)      Noela Remy – Manyara
5)      Elizabeth Boniface – Singida
6)      Amina Mgoo – JKT / Arusha
 
Timu ya Relay Wanaume wawili;
1)      Faraja Damas – JKT / Arusha
2)      Marco Sylvester – Singida
Timu ya Relay Wanawake wawili, itangazwa hivi karibuni kutokana na sababu za kiufundi.
 
Makocha wa timu ya taifa;
Kamati ya Ufundi ya RT, imewapendekeza wafuatao kuwa makocha wa timu hii ya Taifa.
 
1)      Naasi Gwagwe Dengwe – CCP
2)      Thomas John Tlanka– Arusha
3)      Francis Nade – Manyara
4)      Zakaria Barie – Arusha
5)      Lwiza John – Mbeya
Kwanza nawapongeza Viongozi wakuu wa RT nikianza na Rais wa Shirikisho Mh. Anthony Mtaka kwa maono yake, bidii za kutafuta namna yoyote ya kuendeleza mchezo wa riadha, suala la kutoa zawadi kwa washindi katika mashindano ya mwaka huu ni wazo lake na ndiyo hali iliyoleta hamasa zaidi.
Pia suala la kuendesha mashindano mikoani kikanda, pia ni wazo lake, sisi wengine tuliweka ‘strategies’ ili ‘idea’ ile ikae kiufundi zaidi.
 
Pia kwa uamuzi wake wa kipekee, kuamua kuwalipia ada ya ushiriki wa mbio za Kilimanjaro Marathon, wanariadha wote walioshiriki mbio za Nyika za Taifa kwa categories zote na kushika nafasi kumi za juu.
 
Napenda pia kuwashukuru Makamu wa Kwanza wa Rais RT ambaye pia ni Mwenyekiti Kamati ya Fedha, Ndg. William Kallaghe kwa kufanikisha ‘Transaction’/pesa mapema, Makamu wa Pili wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti Kamati ya Ufundi, Dk. Ahmad Ndee kwa kusimamia taratibu zote za kiufundi, Mama Rehema Killo (Katibu Kamati ya Ufundi), kwa kusimamia ‘logistics’ zote za kiufundi.
 
Bila kumsahau Mwenyekiti Kamati ya Mbio za Nyika na Barabara (CC &RR) Ndg. Meta Petro, Tullo Chambo – Mjumbe wa Kamati Tendaji na Mwenyekiti Kamati ya Habari na Mahusiano, wanariadha wakongwe wa zamani Zakaria Barie, Lwiza John, Robert Kalyahe ambao Wajumbe wa Kamati Tendaji na pia ni wajumbe wa Kamati ya Ufundi, ambao walijitolea kufanya kazi kwa bidii hadi kikaeleweka, wakishirikiana kwa karibu na Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro (KAA).
 
Nwashukuru pia wajumbe wa Kamati Tendaji ambao walitupa ushirikiano wakiwa makao makuu, Katibu Mkuu Msaidizi Mama Ombeni Zavalla kwa nasaha zake, Mwinga Mwanjala na Super Star Mjumbe wa Shirikisho la Riadha Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, na  Katibu Mkuu Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Meja mstaafu Filbert Bayi, Peter Mwita (Starter wa Kimataifa), na Mjumbe wa Kamti Tendaji, Mzee Christian Matembo kutoka Songea.
 
Kwa namna ya kipekee kabisa naomba pia niwapongeze MKURUGENZI WA MASHINDANO Ndg. Robert Kalyahe kwa kuongoza mbio kitaalamu na Mweka Hazina Gabriel Liginyan, kwa kuhakikisha malipo yote yanakwenda sawa.
 
Nje ya kamati tulikuwa na bingwa mara mbili wa Jumuiya ya Madola Mzee Gidamis Shahanga, Alfredo Shahanga, rais mstaafu Francis John bila kusahau wataalam waliopima njia kisomi kabisa – John Bayo, Anthony Mwingereza na Naasi Gwage.
 
Kamati maalum ya Cross Country Series tunawapa pongezi kwa ubunifu mzuri.
 
Aidha, pongezi za kipekee zimwendee Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Riadha Mkoa wa Singida, Miraji Jumanne Mtaturu, kwa ushirikiano wake mkubwa katika maendeleo ya riadha, ikiwamo kujitolea kufanikisha mashindano ya wazi kwa mikoa ya kanda ya kati ya vijana, ambayo yatafanyika mwezi ujao maalumu kupata timu ya Taifa ya Vijana kwa ajili ya mashindano ya vijana ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, ambako Tanzania itakuwa mwenyeji.
 
Kwa unyenyekevu mkubwa, tunawaomba watanzania kwa ujumla kutupa sapoti kwa ajili ajili ya maandalizi ya Timu hii ya Taifa ya Nyika, ikiwamo kambi ambayo itaanza mara baada ya mashindano ya Mbio za Kilimanjaro Marathon mjini Moshi.

No comments:

Post a Comment