Tuesday 21 February 2017

Mugabe: Sikutaka Trump au Clinton washinde Urais Marekani

 
Umoja wa Ulaya(EU) umeongeza muda wa vikwazo kwa Rais Robert Mugabe na Mkewe, Grace kwa mwaka 1 hadi Februari 20, 2018.
Hata hivyo Rais Mugabe amesema kuwa hakutaka Donald Trump awe rais wa Marekani lakini pia hakupenda Bi. Clinton ashinde kwakuwa angekuja kuendeleza vikwazo kwa nchi yake.

Rais Mugabe Leo anatimiza miaka 93 na kuwa rais mwenye umri mkubwa zaidi Duniani. Alizaliwa mnamo mwaka 1924 pia aliwahi kufungwa jela mwaka 1964 na kutoka mwaka 1974 kwa kosa la kutoa hotuba ya kuihujumu Serikali.

No comments:

Post a Comment