Tuesday 21 February 2017

Uhakiki wa vibali ya kufanyia kazi kwa wageni


images
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu pamoja na mambo mengine ina jukumu la kusimamia na kuratibu ajira za wageni nchini. Hii inajumuisha kupokea na kushughulikia maombi ya vibali vya kufanya kazi nchini kwa wageni na kutoa vibali husika.
Katika kipindi cha hivi karibuni imebainika kwamba kuna baadhi ya waajiri na wageni kwa kujua ama kwa kutokujua wanakiuka masharti yaliyoainishwa na Sheria ya Kuratibu Ajira za wageni Na. 1/2015. Tabia hii imekuwa ikifanywa na baadhi ya waajiri na madalali wanaowatumia.
Ofisi inawajulisha waajiri wote kwamba, mfanyakazi wa Kigeni kufanya kazi bila kibali cha kazi kilichotolewa na Kamishna wa Kazi ni kosa la jinai. Hivyo, waajiri wote wanapaswa kuzingatia kuwa wafanyakazi wao wa kigeni wanakuwa na vibali halali vya kazi.
Ofisi inawajulisha waajiri kwamba kutakuwa na ukaguzi maalumu wa kuhakiki vibali vya kufanya kazi nchini ili kuhakikisha kuwa wageni wote wanaofanya kazi wana vibali halali vya kazi. Hivyo, wageni wote wanaofanya kazi nchini wanapaswa kuwasilisha vibali vyao katika Ofisi za Kazi za kila Mkoa kwa ajili ya uhakiki ndani ya siku 30 toka tarehe ya tangazo hili.
Kamishna wa Kazi anatoa rai kwa waajiri na wageni wote wanaofanya kazi nchini kushiriki kikamilifu katika zoezi hili la kuhakiki vibali ili kuepuka usumbufu wowote usio wa lazima.
Imetolewa na;
KAMISHNA WA KAZI
     OFISI YA WAZIRI MKUU
  KAZI, VIJANA, AJIRA  NA WENYE ULEMAVU                
22/02/2017

No comments:

Post a Comment