Tuesday 21 February 2017

Neymar anakaribia kuhukumiwa

Sasa ni wazi kwamba mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Barcelona Neymar Do Santos anakaribia kuhukumiwa. Hukumu ya Neymar inakuja baada ya mahakama nchini Hispania kuamua kutupilia mbali rufaa ya kupingwa kutolewa kwa hukumu iliyoletwa na mawakili wa mchezaji huyo.
Neymar anakabiliwa na kesi ya kuficha kiasi halisi cha pesa iliyotolewa na Barcelona wakati wakimnunua toka Brazil.Uhamisho wa Neymar kwenda Barcelona ulikuwa na mambo mengi huku kampuni toka Brazil iitwayo DIS wakidai kuzungukwa na Neymar pamoja na baba yake katika usajili huo.
Inadaiwa Neymar na baba yake walisema kiasi walichopewa na Barcelona ilikuwa £40m tu, lakini taarifa zinasema Neymar na baba yake walikula zaidi ya £79m na walijaribu kushusha kiwango hicho ili kutowalipa DIS na hii iliifanya kampuni hiyo kumshtaki Neymar na baba yake.
Sasa mahakama imeamua kuendelea kusikiliza shauri hilo.Upande wa mlalamikaji wamesisitiza kwamba kuna rushwa ilitawala katika tukio zima la uuzwaji wa Neymar.Mahakama imeombwa kutoa adhabu ya kuanzia miaka miwili kutokana na ukubwa wa kesi hiyo.

Kesi hii ilianza toka 2013 japokuwa haijamuathiri Neymar uwanjani. Sasa mwisho wa kesi umekaribia japokuwa kifungo cha miaka chini ya miwili jela na faini ya £10m vitamfanya atumikie kifungo cha nje kutokana na sheria ya nchi hiyo inavyosema.

No comments:

Post a Comment