Saturday 25 February 2017

Watu 7 wamefariki dunia kutokana na mvua kubwa ilionyesha

Watu saba wamefariki dunia wilayani Arumeru katika matukio tofauti yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha usiku wa kuamkia  leo (Februari ishirini na nne )
Akielezea matukio hayo kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa  Arusha  DCP Charles Mkumbo amesema tukio la kwanza ambalo limepoteza maisha ya watu watano limetokea katika kata ya Enaboishu baada ya  gari aina ya Toyota Premio lenye namba za usajili T 579 BSG kusombwa na maji.
Yusuph Jacob ndiye aliyekua dereva wa gari lililosombwa na maji wakiwa wanatoka kwenye sherehe za kukabidhiwa mwali anasema baada gari kuzidiwa na maji alilazimika kuegesha gari lakini maji yalizidi nguvu.

Baadhi wa mashuhuda walioshuhudia tukio hilo wanasema ushirikiano wa wananchi umesaidia kupatikana kwa miili yote ambayo imehifadhiwa kwenye nyumba ya kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru.

No comments:

Post a Comment