Saturday 25 February 2017

Kaburu afunguka asema Simba wasiwe chanzo cha fujo leo

Makamu wa Rais wa klabu ya Simba SC, Godfrey Nyange Kaburu.
Makamu wa Rais wa Simba Godfrey Kaburu amefunguka na kuwataka mashabiki wa klabu ya Simba kutokuwa chanzo cha vurugu na fujo zozote katika uwanja wa Taifa katika mechi yao leo dhidi ya watani wao wa jadi Yanga kwani fujo zinarudisha nyuma klabu hiyo.
Godfrey Nyange Kaburu akiongea na EATV amesema kuwa anaamini mashabiki wa Simba ni wastaarabu na wanaipenda klabu yao hivyo wasiwe sehemu ya kuirudisha nyuma klabu hiyo

"Klabu ya Simba inapiga vita fujo na haipendelei kuona fujo zozote zile uwanjani pale leo, kwa sababu fujo zozote zile zinapelekea kurudisha nyuma maendeleo ya klabu kwa mfano utaona kutokana na fujo za kipindi kile tulipata adhabu kadhaa,  klabi imetumia pesa nyingi kugharamia miundo mbinu ile ambayo iliharibiwa na mashabiki wetu, lakini pia mmeona tulisimamishwa kwa muda kutumia Uwanja wa taifa, kwa ustarabu ambao Simba wanao si jambo jema sisi kuonekana ni vyanzo vya fujo, Simba ni watu wastarabu, watu wanapenda mchezo, ni watu ambao wanapenda klabu yao" alisisitiza Kaburu
Mbali na hilo Kaburu amewataka mashabiki kujiandaa kupokea matokeo ya aina yoyote ile kwa ustaarabu na kuepukana na fujo ambazo zinaweza kuirudisha nyuma tena klabu yao

No comments:

Post a Comment