Saturday 16 July 2016

Wimbo ‘Pale Kati Patamu’ wa Nay wa Mitego wafungiwa rasmi

 
Na Chrispino Mpinge

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa ‘pale kati patamu’ ulioimbwa na msanii Nay wa Mitego kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza ameeleza kuwa msanii huyo amekuwa na tabia na mienendo yenye kuchafua sekta ya sanaa yeye binafsi kupitia kutoa kazi chafu na kufanya maonyesho yenye kukiuka maadili.


“Kazi zake zikikiuka maadili na kudhalilisha utu wa mwanamke sambamba na kutoa lugha za matusi na za kudhalilisha watu wa kada mbalimbali.” alisema Mngereza.

Aliongeza, “Ikumbukwe kwamba BASATA limeshamuita na kumuonya msanii huyu mara kadhaa kutokana na tabia yake ya kutoa kazi zisizokuwa na maadili na aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio haya kwa makusudi ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu kazi ya sanaa kama kazi nyingine. Kwa sasa Msanii huyu ametoa wimbo mwingine wa ambao uko mitandaoni ukipambwa na picha chafu zinazoonesha mwanamke akiwa mtupu yaani uchi wa mnyama.

No comments:

Post a Comment