Tuesday 26 July 2016

Arsenal wanahitaji zaidi ya Sanchez na Ozil : Collymore

Arsenal wanahitaji kufanya usajili zaidi kutokana na kukosa wachezaji wenye ubora wa juu huku Mesut Ozil, Alexis Sanchez na Granit Xhaka wakisemwa kwamba si wazuri kwa kiwango hicho, hii ni kwa mujibu wa Stan Collymore.
Arsene Wenger amemsajili Xhaka pekee kwenye dirisha hili la usajili huku akisisitiza kwamba yuko tayari kutumia pesa kusajili isipokuwa kwa wachezaji sahihi tu kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Arsenal tayari wamewakosa Jamie Vardy huku Gonzalo Higuain akitajwa kuwa njiani kujiunga na Juventus, na hivyo basi, Collymore anahisi kwamba kuna uhitaji mkubwa wa klabu hiyo kufanya usajili wa maana zaidi ili kuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa kwenye mbio za kuwania taji la ligi la msimu ujao.

“Bado naamini kwamba timu hii ya Wenger itakuwa katika nafasi nne za juu endapo tu watasajili beki wa kati mzuri na mshambuliaji wa kati mzuri, vinginevyo sidhani kama watakuwa na fursa hiyo,” ameandika kwenye gazeti la Sunday Mirror.

“Kwamba, kwa timu ambayo mawazo yake makubwa ni kupata nafasi ya kushiriki Michuano ya Uefa kila msimu, hii litakuwa ni janga kubwa.

“Ni ukweli ulio wazi kwamba timu ya Wenger ina huo uhitaji, lakini bado anaonekana kuwa mbishi kutumia fedha ambazo hata hivyo si zake, unaweza kuona kwamba wakati wa Arsenal ya Sol Campbell, ukuta ulikuwa hauoenyeki kirahisi.

“Vile vile bado sioni kama Mesut Ozil, Alexis Sanchez au Granit Xhaka ni wachezaji wa viwango vya juu kiasi hicho. Kweli ni wachezaji wazuri. Xhaka ni usajili sahihi, ni mchezaji ambaye ni katili uwanjani lakini vile vile ananyumbulika.

“Lakini hata hivyo usajili huu hauna maana kwamba Arsenal ndio wamemaliza kama ambavyowenzao wamemleta mtu kama Zlatan Ibrahimovic na sasa mbioni kuleta mtu kama Paul Pogba.

“Kama Wenger angemleta Suarez wakati ule, sasa angekuwa anapiga goli za kutisha kuliko hata anavyofanya kunako klabu ya Barcelona,” amemaliza.

No comments:

Post a Comment