Sunday 31 July 2016

Kamati ya utendaji Chadema Moshi yavunjwa

Moshi. Baraza la uongozi la Chadema mkoa Kilimanjaro limeivunja kamati ya utendaji ya chama hicho wilaya ya Moshi mjini, inayoongozwa na Mbunge wa moshi Mjini, Jaffar Michael.
Uamuzi wa kuivunja kamati hiyo umo katika barua ya mwenyekiti wa Chadema mkoa Kilimanjaro, Philemon Ndesamburo kuwa umetokana na minyukano isiyoisha ndani ya kamati hiyo.


Akizungumzia huo, Michael amelithibitishia gazeti hili kuvunjwa kwa kamati yake ya utendaji iliyokuwa na wajumbe 12 akisema ameupokea kwa moyo mkunjufu.


“Uamuzi huo nimeukubali na nimeupokea kwa moyo mkunjufu na unyenyekevu mkubwa kwa ajili ya maslahi mapana ya chama chetu ambacho nimekipigania kwa akili zangu zote na nguvu zangu zote,” amesema.

No comments:

Post a Comment