Friday 29 July 2016

Davido ageukia kusomesha wanafunzi

Staa wa muziki kutoka Naija, David Adeleke ‘Davido’ amesema kuwa ameingia rasmi katika kusomesha wanafunzi ili waweze kujikwamua kimaisha.
Davido ambaye baba yake naye alishawahi kusomesha wanafunzi 200 miaka ya nyuma, alisema kuwa mipango yake ni kusomesha wanafunzi kupitia mradi maalum wa mama yake, Veronica.

“Vijana wengi wanastahili kupata elimu.

Mwaka huu nitaanza kusomesha wanafunzi kupitia mradi wa mama yangu uitwao Veronica Education Scholarship Program. Nitakuwa nawasomesha wanafunzi bure kila mwaka. Mwaka huu nitaanza na wanafunzi wanne,” alisema Davido.

No comments:

Post a Comment