Sunday 31 July 2016

Wanafunzi wapewa Adhabu ya kung'oa Kisiki cha Mti uliopandwa na mkolon

Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu KATOKE ( TTC ) kilichopo Kagera Wilaya ya Muleba walalamika juu ya adhabu wanazopewa na uongozi wa hapo Chuoni pindi wanapofanya makosa..
Mwanafunzi akieleza hali ya Shuleni hapo..
Mnamo tarehe 27/07/2016 saa 3:28Pm kengele iligongwa kwa ajili ya kwenda paredi ambapo huwa ni siku ya (EK) Yaan elimu ya kujitegemea ambapo huwa tunatakiwa kwenda paredi kwa ajili ya kugawiwa majukumu ya kazi. Kengele inapaswa igongwe saa 3:30pm au saa 4:00pm inategemeana na ratiba ya siku ila inayofahamika ni saa 4:00pm kwa siku ya jumatano. 

Tulichelewa dakika 1 tu paredi basi ikawa ni kosa na ndipo ikasababisha tukapewa adhabu kama zifuatazo:- 1 kuandika barua kwanini tumechelewa paredi. 2 tukapewa fomu ya mashitaka, ambapo fomu hii huwa mpaka kamati ya Nidhamu ijadili na ndipo itolewe tena kwa kosa kubwa aidha umesimamishwa masomo ila sisi tulipewa fomu ya mashitaka bila hata kamati ya nidhamu kukaa. 3 Tukapewa adhabu ya kung'oa GOGO ambalo mtii ulipandwa miaka mingi sana iliyopita pindi chuo kipo kwa matumizi ya kikoloni na hayo magogo au visiki mizizi yake kwa ukubwa unapasua mbao. 4 mwalimu aliyetupa adhabu kawatoa baadhi ya wasichana katika adhabu. 5 Aliahidi atatuandika katika black book. 

Kwa mjibu kosa haliendani na adhabu aliyotoa kwani hata tungeandika barua ilikuwa ni adhabu tosha. katika adhabu tulikuwa 30 ila kwa sasa tuko 23 ambapo kila kisiki kina watu 8 na wengine wanafyeka msitu mnene kweli. Binafisi sisi tumechukizwa sana pia rais wa chuo hana sauti. Hivi visiki hata tukichimba mwezi labda ndio vitakamilika ila module zitakuwa zimetupita na usomaji utakuwa wa taabu. Tunaomba mtusaidie ili haki itendeke pia kuna MICHANGO YA KIHOLELA WANATUCHANGISHA HALAFU HATUELEWI MANUFAA YAKE MANA TUKIHOJI HAWASEMI WAZI. CHUO CHA UALIMU KATOKE-BUKOBA.

No comments:

Post a Comment