Saturday 16 July 2016

​Rihanna asitisha show ya Nice, Ufaransa kufuatia mauaji ya watu 84

Rihanna amelazimika kusitisha show yake ya ziara ya dunia ya Anti jijini Nice, Ufaransa kufuatia mauaji ya watu 84  Alhamis hii.
Muimbaji huyo alikuwa atumbuize kwenye uwanja wa Allianz jijini humo.

Alitangaza hatua hiyo kwenye Instagram:

 


Kwenye tukio hilo watu wengine 202 walijeruhiwa.

Ijumaa hii maafisa wa Ufaransa walimtambua mtu aliyehusika kwenye mauaji hayo ambapo alitumia gari lenye tani 19 kuwagonga watu hao waliokuwa wamejazana kwenye sherehe za Bastille Day.

Mtu huyo, Mohamed Lahouaiej Bouhlel 31, anadaiwa kuwa raia wa Tunisia mwenye historia ya uhalifu mdogo na matatizo kwenye ndoa yake.

No comments:

Post a Comment