Wednesday 27 July 2016

CHADEMA wametangaza operesheni ya kupambana na udikteta Tanzania UKUTA


IMG-20160727-WA0160.jpg IMG-20160727-WA0161.jpg
IMG-20160727-WA0173.jpg
IMG-20160727-WA0174.jpg

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO <CHADEMA>
MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAMATI KUU ILIYOFANYIKA HOTELI YA BAHARI BEACH LEDGER PLAZA JULAI, 2016.

1.0 UTANGULIZI
Kamati Kuu ya dharura ya Chama iliketi kuanzia 23-26 Julai ,2016 Jijini Dar es salaam na ilikuwa na ajenda moja mahsusi ambayo ni kujadili hali ya siasa na uchumi wa Taifa tangu serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani mwenzi Novemba ,2015.
Mwenendo wa serikali hii ya CCM ya awamu ya tano ,chini ya Raisi John Magufuli ,ni dhahiri kuwa umeamua kuiweka demokrasia kizuizini na kuleta utawala wa Kidektteta katika nchi yetu.


2.0 MATUKIO MAHSUSI YA UKANDAMIZAJI WA HAKI NA DEMOKRASIA NCHINI

2.1-Kupiga marufuku mikutano ya Vyama vya siasa.
Serikali kupitia Waziri Mkuu hatimaye Raisi na jeshi la Polisi walitangaza kwa nyakati tofauti kwamba ni marufuku kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa mpaka mwaka 2020 ili kuipa serikali nafasi ya kufanya kazi.Huu uvunjaji wa Ibara ya 20 <1>ya Katiba.

Aidha katazo hilo la mikutano ya siasa linakiuka Sheria namba 5 ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 kifungu cha 11 ambayo imetoa haki kwa vyama vya siasa kufanya kazi ya siasa.

2.2 Kupiga Marufuku urushaji wa moja kwa moja <live coverage>wa mijadala ya bunge .Katazo hilo ni kinyume na Katiba ibara ya 18 ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambayo inatoa uhuru wa maoni na uhuru wa kupata habari kwa kila mwananchi .

2.3 Kudhibiti Wabunge wa Upinzani bungeni -Serekali imejificha nyuma ya kiti cha Naibu Spika wa bunge ,Dkt.Tulia Ackson Mwansasu <Mb> ili kuwathibiti wa upinzani Bungeni kwa lengo la kuwanyamazisha wasiikosoe serikali.

Ikumbuke kwamba Dkt.Tulia akiwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa mtumishi wa umma asiyepaswa kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa;lakini ghafla anaonekana akigombea nafasi ya Naibu Spika kupitia CCM.Hivyo yupo Naibu Spika ambaye ni mteule wa Rais.Swali Anawajibika kwa nani kati ya Bunge na Raisi?

No comments:

Post a Comment