Friday 29 July 2016

Hawa ndo mahasimu katika vilabu vyao



 10. PJANIC & DZEKO, Bosnia
 Wawili hao ni wachezaji wa timu ya taifa ya Bosnia walikuwa pamoja kwenye kikosi cha Roma hadi pale Pjanic alipohamia Juventus hivi karibuni.

Dzeko na Pjanic walikuwa ni msaada mkubwa ndani ya Roma, lakini kuanzia msimu huu watacheza wakiwa wapinzani kutokana na Pjanic kujiunga na ‘kibibi kizee cha Turin’ huku Dzeko akiendelea kusalia Roma.

9. ZABALETA & ROJO, Argentina
 Pablo Zabaleta amekuwa akiitumika Man City tangu mwaka 2008 na amefanya kazi nzuri hadi sasa. Rojo alijiunga na United misimu miwili iliyipita lakini bado hajaonesha uwezo mkubwa kuwashawishi mashabiki wa ‘Mashetani wekundu’.

8. MARTIAL & GIROUD, France
 Martial alijiunga na Manchester United msimu uliopita na kwa haraka akafunga magoli muhimu kwa timu yake, huku Olivier Giroud akiwa ndiye mshambuliaji muhimu kwa Arsenal kw sasa.

7. KEVIN DE BRUYNE & FELLAINI, Belgium
De Bruyne na Fellainini wachezaji kutoka vilabu viwili hasimu zaidi vya jijini Manchester ambao wanaheza pamoja kwenye timu taifa. De Bruyne akiwa Manchester United wakati Fellainini yeye anaitumikia klabu ya Manchester United.

6. PISZCZEK & LEWANDOWSKI, Poland

Wapoland hawa wawili walikuwa pamoja pia kwenye klabu ya Borussia Dortmund kabla ya Lewandowski kuamua kuihama klabu hiyo na kuhamia Bayern Munich.


5. MODRIC & RAKITIC, Croatia

Hawani viungo mafundi wa timu ya taifa ya Crpatia ambao hukutana kwenye pambano la El Clasico linalovihusisha vilabu viwili hasimu zaidi katika historia ya soka la Hispania. Modric  akiwa upande wa Real Madrid wakati Rakitic anaiwakilisha Barcelona.

4. ROONEY & STURRIDGE, England

Watoto hawa wa taifa la England wamekuwa na mchango mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji ya timu yao ya taifa kwa miaka kadhaa sasa.

Lakini inapofikia kwenye ngazi ya vilabu, wawili hawa wanageuka na kuwa maadui wakubwa linapopigwa pambano linalozihusisha Liverpool anayoichezea Sturridge dhidi ya Manchester United inayowakilishwa na Rooney.

3. SCHWEINSTEIGER & OZIL, Germany 

Bastian alisaini kujiunga na Manchester United msimu uliopita na kukutana na mjerumani mwenzake Ozil anayekipiga England kwenye klabu ya Arsenal. Bastian amerejea kutoka majeruhi wakati Ozil ni mchezaji muhimu kwa upande wa Arsenal, itavutia san kushuhudia namna ya wajerumanin hawa watakavyofanya pale klabu zao zitakapokutana msimu huu.


 2. MARCELO & NEYMAR, Brazil

Real Madrid v FC Barcelona ni game yenye upinzani mkubwa sana kwenye ligi ya Hispania si tu kwasababu vilabu hivi vinamajina makubwa nchini humo, bali pia ni kutokana na vikosi vya timu hizi kuundwa na wachezaji wenye uwezo wa hali ya juu na wenye majina makubwa kwenye ulimwengu wa soka.

Marcelo akiwa Real Madrid na Neymar akiwa Barcelona, wote wanacheza timu ya taifa ya Brazil lakini inapofika katika ngazi ya klabu kila mmoja anapambana kuhakikisha timu yake inapata ushindi na kuibuka na vikombe mbalimbali.


No comments:

Post a Comment