Saturday 30 July 2016

Rais wa Uturuki awasamehe waliomtukana

Rais Tayyip Erdogan

Rais Erdogon wa Uturuki ametangaza msamaha kwa watu wote waliokabiliwa na mashtaka ya kutukana, katika kile alichotaja kama ishara ya heri njema.
Zaidi ya watu 2,000 walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kumtukana Rais kwa muda wa miaka miwili iliyopita.
Akizungumza katika hafla katika mji mkuu wa Ankara kuwakumbuka zaidi ya watu 200 wanaodaiwa walifariki katika jaribio la mapinduzi, rais Erdogon aliyakebehi mataifa ya Marekani na Ulaya.

Alisema wale watu wanaowajali zaidi watu waliotekeleza jaribio la mapinduzi kuliko wanavyojali demokrasia ya taifa hilo si marafiki wa Uturuki.

Awali kamanda wa Marekani katika eneo hilo , Jemedari Joseph Votel, alitaja lawama za Bwana Erdogon kama za kusikitisha na zisizo na ukweli wo wote.

No comments:

Post a Comment