Friday 29 July 2016

Suzan Kiwanga na Peter Lijualikali, Wameshinda kesi za Uchaguzi katika Majimbo yao


Leo ni hukumu kesi ya kupinga matokeo ya ubunge jimbo la Kilombero na Mlimba.
Kutokana na majimbo hayo kuwa na historia ya Vurugu zinazotokana na matukio ya kisisasa, jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi mkali katika viwanja ya ukumbi wa Halmashauri ya Kilombero inakosikilizwa kesi ya mbunge wa jimbo hilo na katika mahakama ya wilaya, inakosikilizwa kesi ya mbunge wa jimbo la Mlimba.

Kesi ya Kilombero na Mlimba zinasikiliziwa Sehemu moja.

12195769_639930579481770_219738213110648768_n.jpg
Mbunge wa jimbo la Mlimba Mkoa wa Morogoro, Suzan Kiwanga (CHADEMA)

13882551_1772776119626635_5361149175275392023_n.jpg
Mbunge wa Jimbo la Kilombero Peter Lijualikali (CHADEMA)
1. Mh. PETER AMBROS LIJUALIKALI ametangazwa kuwa Mbunge halali wa Ifakara mjini.

Sababu za  Ushindi; 




  • Mashahidi Kujichanganya.
  • Kutopeleka Malalamiko Kamati ya Maadili.
2. Mbunge wa jimbo la Mlimba kupitia CHADEMA Suzan Kiwanga, ameshinda kesi ya uchaguzi katika Mahakama Kuu ya Mkoa wa Morogoro.
13880217_10154457768056473_672013077803494133_n (1).jpg
Mawakili waliosimamia Kesi za Suzan pamoja na Peter.

Katika Uchaguzi mkuu wa 2015 Jimbo la Mlimba, Suzan Kiwanga alishinda kwa kupata kura 40,068 dhidi ya Mpinzani wake wa karibu Godwin Kunambi wa CCM aliyepata kura 34,883.

Jimbo la Kilombero Peter Lijualikali wa CHADEMA alishinda kiti cha ubunge kwa kupata kura 62,158 wakati mpinzani wake wa karibu, Abubakar Assenga wa CCM alipata kura 44,092.

No comments:

Post a Comment