Thursday 28 July 2016

Mpiga picha mkuu wa Tanzania Daima Joseph Senga amefariki dunia


 
 mpiga Picha mkongwe wa Gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga, amefariki dunia.
Senga alipelekwa nchini india humo kwa matibabu ya moyo, ambapo tayari alikwisha ruhusiwa baada ya matibabu na kurejea hotelini kwake kwa mapumziko na kujiandaa na safari ya kurejea nchini.


Kabla ya kifo chake imeelezwa kuwa Marehemu alizungumza na mkewe kwa njia ya simu akimueleza kuwa hali yake ni nzuri na anaendelea vizuri na kwamba alitarajia kuanza safari ya kurejea nchini mnamo tarehe 5/8/2016 na alitarajia kufika Tanzania tarehe 6/8/2016.

Imeelezwa kuwa baada ya maongezi hayo kwa simu aliomna msaada akaogeshwe kutokana na mkono wake mmoja kushindwa kukunjika kutokana na Operesheni hiyo.

 Hali ya Marehemu ilianza kubadilika na baadaye kati ya saa 12 na saa 1 jioni ya jana na kurudishwa Hospitalini. 

Wakiwa njiani hali yake ilizidi kubadilika na baada ya kufika Hospitalini hapo Madaktari walimpima na kuthibitisha kuwa tayari alikwishafariki dunia. MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU JOSEPH SENGA MAHALA PEMA PEPONNI, AMEEN





No comments:

Post a Comment