Wednesday 27 July 2016

Mwambusi amezungumzia kiwango cha Chirwa

Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi

Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga Juma Mwambusi amevunja ukimya na kutoka ufafanuzi kuhusu watu wanaobeza kiwango cha mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia Obrey Chirwa aliyesajiliwa na klabu hiyo hivi karibuni.
Wadau wengi wa soka nchini ikiwa ni pamoja na baadhi ya mashabiki wa Yanga wamekuwa wakihoji uwezo wa nyota huyo aliyesajiliwa akitokea klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe.

“Ni moja ya wachezaji wazuri wa Yanga ambao wameongezwa lakini kwa muda aliocheza bado hajazoea mfumo kwasababu kila klabu imacheza kwa mfumo wake kwahiyo anatakiwa endane na mfumo wetu kwanza. Chirwa ni mgeni Yanga, anatakiwa kuzoea mazingira na mfumo wa mwalimu na anazoea taratimu tuwe na subira,” alifafanua Mwambusi wakati alipofanyiwa mahojiano na kipindi cha michezo cha Sports Extra cha Cloud FM.

“Tumemuona anamuelekeao, tumpe muda atakuwa kwenye kiwango kizuri baada ya muda. Alivyokuja Ngoma mwazoni watu waliona kama hawezi lakini alikuja kufanya kazi nzuri baadae.”

“Yanga imeingia kwenye makundi kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu. Lakini watu wanataka matokeo, hapohapo tupate kombe na kila kitu, ikitokea ndiyo lengo letu kubwa sisi waalimu na wachezaji kupata matokeo mazuri lakini kama ikishindikana basi inatusaidia kupata uzoefu.”

Hadi sasa Chirwa amecheza mechi tatu akiwa na Yanga, mechi ya kwanza ilikuwa dhidi ya TP Mazembe kwenye uwanja wa taifa, akacheza tena dhidi ya Medeama Yanga ilipokuwa kwenye uwanja wa taifa kabla ya kucheza tena dhidi ya Medeama katika mchezo wa marejeano jana nchini Ghana.

No comments:

Post a Comment