Friday 29 July 2016

Wizara ya Nishati na Madini imetoa semina ya siku moja kwa Wakuu wa Mikoa ambayo Bomba la Mafuta litapita kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga

MHO1Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akizungumza wakati akufungua semina  siku moja kwa Makatibu Wakuu wa Wizara zinahusika moja kwa moja na ujenzi wa Bomba la Mafuta na Wakuu wa Mikoa ambayo  Bomba hilo linapita kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.
MHO2Sehemu ya Makatibu Wakuu wa Wizara zinahusika moja kwa moja na ujenzi wa Bomba la Mafuta na Wakuu wa Mikoa ambayo  Bomba hilo linapita kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania wakati wa semina ya siku moja juu ya ujenzi wa bomba hilo.
MHO3Sehemu ya Makatibu Wakuu wa Wizara zinahusika moja kwa moja na ujenzi wa Bomba la Mafuta na Wakuu wa Mikoa ambayo  Bomba hilo linapita kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania wakati wa semina ya siku moja juu ya ujenzi wa bomba hilo.
MHO4Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa( kulia) katika mahojiano ya mubashara( live) na Kituo cha Televisheni cha Taifa (TBC 1), na Mtangazaji wa kituo hicho Anna Kwambaza( kushoto)

Na Zuena Msuya, Dar Es Salaam
Wizara ya Nishati na Madini imetoa semina ya siku moja kwa  Wakuu wa Mikoa ambayo Bomba la Mafuta litapita kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania na Makatibu Wakuu wa Wizara zinahusika moja kwa moja na Ujenzi wa Bomba  hilo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo jijini Dar es salaam, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter amesema, semina hiyo itawawezesha Viongozi hao kuwa na uwelewa mpana juu ya ujenzi wa bomba hilo pia kushirikiana kwa karibu na kufanikisha kukamilisha mradi wa bomba hilo kwa wakati uliopangwa.


Aidha, amesema endapo wahusika wakuu watafahamu kwa kina mwenendo mzima wa ujenzi bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda hadi  bandari ya Tanga hapa nchini, hali hiyo itasaidia kutoa elimu zaidi kwa wananchi na hivyo kuondoa changamoto mbalimbali zilizowahi kutokea wakati wa utekelezaji wa miradi mingine mikubwa iliyotangulia.
Profesa Muhongo ametaja baadhi ya Wizara ambazo zina husika moja kwa na ujenzi wa bomba hilo kuwa ni pamoja na Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi,Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi pamoja na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Wizara zingine ni pamoja na Wizara  ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Mradi wa ujenzi wa Bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania utakuwa Mradi wa tatu kwa Ukubwa nchini Tanzania ukitanguliwa na ule wa Ujenzi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Tanzania hadi Zambia( TAZARA) na Ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Mkoa Mtwara hadi Jijini Dar es salaam.
Bomba hilo litakuwa na urefu wa kilomita 1,443 na upana wa nchi 12, litagharimu shilingi bilioni 3.5 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2020.

No comments:

Post a Comment