Rais Kabila anamaliza muda wake mwishoni mwa Desemba mwaka huu
Kiongozi wa tume ya Umoja wa Mataifa kuhusiana na masuala ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amenukuliwa akisema nchi hiyo huenda isiweze kuandaa uchaguzi wa urais hapo Novemba kama ilivyokuwa imepangwa.
Akitoa matamshi hayo asubuhi ya leo, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters,
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, mkuu wa tume hiyo Maman Sidikou ameambia kikao cha waandishi habari mjini Kinshasa kwamba ''ni raia wa Congo wenyewe ambao wataamua ni lini uchaguzi huo utakapofanyika'.
Maafisa kadhaa katika Umoja wa Mataifa wamekuwa wakionya kwamba kucheleweshwa kwa uchaguzi huo huenda kukazua upya vurugu na rabsha za kisiasa nchini humo.
Moise Katumbi: Serikali ya DRC ilijaribu kuniua
Rais Joseph Kabila anatarajiwa kuondoka madarakani baada ya muhula wake kukamilika.
Hata hivyo, wapinzani wake wasema anachelewesha uchaguzi huo wa Novemba 27 kimakusudi ili aendelee kusalia mamlakani.
No comments:
Post a Comment