Lakini sasa inaonekana kuchoshwa na mvutano wa muda mrefu baada ya kuamua kusema unautambua upande mmoja.
Kumekuwa na mvutano wa muda mrefu katika Klabu ya Stand United kati ya makundi mawili ya Stand United FC na Stand Kampuni.
Awali, TFF ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika Juni 26, mwaka huu baada ya kupokea barua mbili za uchaguzi kutoka makundi hayo mawili ambayo kila moja lilikuwa likitaka kufanya uchaguzi.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, amesema: “Katika kikao kilichofanyika Julai 13, mwaka huu, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imetoa msimamo wake baada ya kupitia vielelezo vyote na kujadiliana na wadau wa Stand United na kugundua kwamba jina la Stand United FC ndiyo jina halali lililosajiliwa na msajili wa klabu na vyama vya michezo hapa Tanzania.
“Uchaguzi uliofanyika hivi karibuni katika Klabu ya Stand United, umebainika kuwa na sifa zote za kuitwa uchaguzi huru na haki kutokana na kuwashirikisha wanachama halali wa klabu hiyo.
“Lakini pia TFF inawatambua viongozi waliochaguliwa kwenye uchaguzi huo na kulitambua daftari la wanachama wa Stand United lililoboreshwa kwa maelekezo ya TFF.”
Katika hatua nyingine, Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF chini ya mwenyekiti wake, Mutabaazi Lugaziya, imeitupilia mbali rufani ya mmoja wa wagombea katika uchaguzi wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma (Dorefa), Kuayawaya Kuayawaya kutokana na rufani yake kuonekana haina mashiko.
Kuayawaya alikata rufaa kwenye kamati hiyo akipinga jina lake kukatwa baada ya kuonekana hana vigezo vya kuwa mgombea katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment