Akiongea na Bongo5, HK amesema, “Hata wakiikataa hii script ya pili tutawapelekea script nyingine.”
“Tumeshapeleka script nyingine zaidi ya wiki tatu zilizopita na nimewapigia simu jana wameniambia bado hata kuipitia bado hawajaipitia. Tulikubaliana na serikali kuwa ni lazima video ya ‘Chura’ ifanyike,” alisema HK.
“Script tuliyowapelekea ni ya kawaida sana, kama wataikataa itabidi tuziweke zote mbili hadharani ili watu wachangie kwa kuwa hata ile ya kwanza haikuwa mbaya, walisema kuwa haina ujumbe kwahiyo kwenye script ya sasa hivi tumezingatia maamuzi yao waliyoyataka kwenye script hiyo,” ameongeza.
Hivi karibuni Snura ameachia wimbo wake mpya ‘Shindu’ ambao unazidi kufanya vizuri kwenye redio na mitaani pia.
No comments:
Post a Comment