Saturday 16 July 2016

Mechi nane kali kabla ya kuanzia kwa msimu mpya

 Achana na ubingwa wa Ureno kwenye michuano ya Euro, sasa ni wakati wa maandalizi wa msimu mpya kwenye ligi mbali mbali barani Ulaya. Mastaa wanarudi kutoka kwenye fukwe za Ibiza tayari kukusanyika kuelekea sehemu mbali mbali za dunia ambapo timu zao zimechagua kufanya maadalizi ya msimu mpya (pre season).

Kuelekea maandalizi hayo kuna utamu wa mechi kali ambazo vilabu vitakutana kabla ya ligi na michuano ya Ulaya kuanza mwezi August. Makala haya inakupa mechi kali nane ambazo zitazihusu timu kubwa ndani ya pre season

Manchester united Vs Manchester City (Beijing National stadium, 25/7/2016)
 Ni derby ya kihistoria ya miamba ya jiji la Manchester nje ya Uingereza, ni mechi ya Jose Mourinho dhidi ya Pep Guardiola kabla ya ligi kuanza. Dunia inasubiri kuona mwanzo wa Zlatan Ibrahimovic ndani ya uzi wa United.

Chelsea vs Liverpool (Rose Bowl Pasadena, 28/7/2016)
Ndani ya jiji la Califonia, ni wakati wa kuiona Chelsea mpya chini ya Antonio Conte kwenye michuano maalum huko Marekani. Jurgen Klopp tayari ameanza kuimarisha safu ya ushambuliaji ya Liverpool kwa kumleta Sadio Mane.
Arsenal vs Manchester City (Ullevi stadium, Gothenburg 7/8/2016)
 Baada ya kelele nyingi za mashabiki wa Arsenal dhidi ya kocha wao Arsene Wenger wakimtaka aondoke zake kisa kukosa taji la ligi kuu kwa miaka 12, ni wakati wake Arsene Wenger kuandaa timu yake pale atapocheza dhidi ya Manchester City.

Tottenham vs Atletico Madrid (Mcg Ground, Melbourne 29/7/2016)

Tottenham Hotspurs baada ya kukosa ubingwa wa Ligi kuu ya England msimu uliopita,
wameimarisha kikosi chao kwa kumsajili Victor Wanyama na Vicent Janssen. Bila shaka wamejiandaa kutorudia makosa ya msimu uliopita ndio maana watacheza na Atletico inayotishia amani ya Barcelona na Real Madrid kwenye ufamle wa La Liga.

Barcelona vs Leicester City (Friends Arena, Stockholm 3/8/2016)
 Mabingwa wapya wa Uingereza, Leicester City dhidi ya mabingwa wa La Liga, FC Barcelona ni mechi ya kuonesha uwezo wa Leicester jinsi itavyoweza kupambana na vigogo nje ya Uingereza pale watapokutana na vigogo hao kwenye michuano ya Ulaya.

Bayern Munich vs Man City (Allianz Arena, Munich 20/7/2016)
 Pep Guardiola atarudi tena kwa mara nyingine kwenye dimba la Allianz Arena kucheza dhidi ya timu yake ya msimu uliopita, Bayern Munich ambayo kwa sasa ipo chini ya Carlo Ancelloti. Bayern wameimarisha safu yao ya ulinzi kwa kuiobomoa safu ya Ulinzi ya Borussia Dortmund baada ya kumsajili Mats Hummels

Real Madrid vs Bayern Munich (East Rutherford, NJ 4/8/2016)
Zinedine Zidane ametwaa ubingwa wa vilabu barani Ulaya msimu uliopita akiwa kocha wa Real Madrid, ni wakati wa kuendeleza kile cha msimu uliopita kupitia mechi hii dhidi ya Carlo Ancelloti ambaye kwa sasa yupo Bayern Munich. Wakati Ancelloti alipokuwa kocha mkuu wa Madrid, Zidane alikuwa kocha msaidizi.

Liverpool vs Barcelona (Wembley, 6/8/2016)
Baada ya kutwaa ubingwa wa nne wa Ulaya kwa kuifunga Man Utd miaka mitano iliyopita, Barcelona itarudi tena kwenye uwanja uleule lakini ikiwa ni maandalizi ya msimu kucheza na Liverpool. Luis Suarez atapata fursa ya kucheza dhidi ya timu yake ya zamani.

No comments:

Post a Comment