Yanga imeendelea kuburuza mkia kwenye kundi lake, ikiwa na pointi moja baada ya kucheza mechi tatu na kupata sare moja dhidi ya Medeama ya Ghana wakiwa nyumbani Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
, Niyonzima alisema ingawa nafasi yao ya kutinga nusu fainali ni finyu lakini watajitahidi kupambana ili angalau waweze kushinda mechi zao tatu zilizobaki za mzunguko wa pili ili kuweka rekodi zao vizuri.
“Ukweli tulicheza tukiwa na presha ya kupata ushindi kwa sababu tuliamini hiyo ndiyo njia pekee ambayo itatufanya tuwe na matumaini ya kucheza nusu fainali na baada ya Madeama kusawazisha bao kama tulipaniki na kujikuta tukicheza bila kufuata yale ambayo kocha ametuelekeza lakini bado tunayo nafasi,”alisema Niyonzima.
Alisema anajua watu wengi wamewatoa kwenye michuano hiyo lakini wao hawawezi kukata tamaa wataendelea kupambana hadi mchezo wao wa mwisho dhidi ya TP Mazembe, kuona kama wanaweza kufanya miujiza na kutinga hatua inayofuata kama ambavyo wamekusudia.
Alisema kupoteza mechi mbili za awali nako kumewafanya kucheza kwa tahadhari sana huku wakitaka kushinda katika michezo inayofuata lakini ugumu wa michuano hiyo nao umekuwa ni moja ya changamoto inayowafanya wazidi kuwa katika nafasi hiyo waliyopo sasa.
Niyonzima aliingia kipindi cha pili kwenye mchezo huo akichukua nafasi ya Amiss Tambwe, na alifanya kazi kubwa kwa kuongeza presha kwenye lango la wapinzani wao Medeama, lakini walishindwa kupata bao la ushindi ambalo lingeweza kuwapaisha hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi hilo.
No comments:
Post a Comment