Shirikisho la soka barani Ulaya
limetangaza majina ya wachezaji 10 watakaowania tuzo ya mchezaji bora
Ulaya kwa msimu wa mwaka 2015/2016, majina hayo 10 yametangazwa huku
Cristiano Ronaldo akipewa nafasi ya kushinda tuzo hiyo itakayotolewa
Agosti 25 mwaka huu.
Majina hayo 10 yametangazwa baada ya
kufanyika mchujo wa majina ya wachezaji 37 ambao walikuwa wamependekezwa
awali na kupigiwa kura, ambapo UEFA imetaja majina ya wachezaji 10
waliofanikiwa kuingia katika kumi bora ikiwa majina 27 ya wachezaji
yaliingia katika kinyanga’nyiro hicho.Majina ya wachezaji hao kumi ni Gareth Bale – Real Madrid, Gian-luigi Buffon -Juventus , Antoine Griezmann - Atletico Madrid, Toni Kroos - Real Madrid , Lionel Messi -Barcelona, Thomas Müller -Bayern Munich, Manuel Neuer - Bayern Munich , Laveran Ferreira Pepe - Real Madrid, Cristiano Ronaldo -Real Madrid, Luis Suarez –Barcelona.
No comments:
Post a Comment