Mbunge wa Segerea, Bonnah Kaluwa
Kaluwa alitoa kauli hiyo jana kwenye Shule ya Msingi Buguruni wakati akigawa madawati zaidi 500 jimboni humo.
Madawati hayo ni yale waliyopewa na Rais John Magufuli hivi karibuni.
Julai 13, Rais Magufuli alizindua mpango wa ugawaji wa madawati 60,000 yaliyotokana na fedha Sh6 bilioni zilizopatikana baada ya Bunge kubana matumizi.
Kaluwa alisema kwa asilimia 95 Segerea imefanikiwa kukabiliana na changamoto za uhaba wa madawati, hivyo kilichobaki ni kupigania ukarabati wa miundombinu ya shule zilizochakaa na masilahi ya walimu.
“Hadi hapa nilipofikia siyo pabaya kwenye kero ya madawati. Sasa hivi nataka nihamishie nguvu zangu kupata ufumbuzi wa masilahi ya walimu na vyumba vya madarasa,” alisema Kaluwa.
Diwani wa Buguruni (CUF), Adam Fugame aliwataka walimu wa shule kuhakikisha madawati yanatunzwa ili vizazi vijazo vitumie.
No comments:
Post a Comment