
DNA
Msanii kutoka nchini Kenya DNA, ametoa sababu iliyomfanya yeye
aimbe wimbo wa 'gospel' na kuzua minong'ono kuwa ameamua kuachana na
Genge na kumuimbia Mungu.
Akiongea kwenye kipindi cha The Cruise ya East Africa Radio, DNA amesema
yeye muziki wake anafanya kadri nafsi yake inavyomwambia, hivyo ana
uhuru wa kuimba kitu chochote na si gospel pekee, kwani hafanyi muziki
kwa ajili ya mashabiki."First of all mi sifanyi muziki kuridhisha mashabiki, nafanya muziki kwa sababu kipaji changu kinanielekeza direction fulani, yani napata idea fulani, hiyo ndiyo inatangulia si kufikiria mambo ya watu wataipokea vipi, kwanza ni ile insipiraion inatoka ndani yangu, na sikutaka kujibana kuimba style moja, so nikasema u know what man, mi namuamini Mungu na najua vile amenifanyia na anaendelea kunitimizia kwenye maisha yangu, so mi nafanya muziki vile mi nafeel, niko na uhuru kwa hii maisha, sijabanwa na mtu, the only thing kinaweza kunibana ni mawazo yangu mwenyewe", alisema DNA.
DNA aliendelea kusema kuwa licha ya hayo anamshukuru Mungu kwani bila yeye angeshapotea kama rafiki zake, ambao wameshapotea kutokana na maisha waliyokuwa wakiishi.
"Mi bado naamini ni mtu wa God, in fact more now than ever, at any time naweza toa ngoma ya kumshukuru Mungu, kwa sababu life style yangu wakati huo ilikuwa life style moja noma sana, alafu pia mabeste zangu na wazee mtaani wamepotea because ya zile vitu tulikuwa tunafanya, so mimi kuwa hai ni sababu Mungu ameamua, ningekuwa nishakufa", alisema DNA.
No comments:
Post a Comment