
Esther ameiomba halmashauri na mkoa kwa ujumla kuwaona kwa jicho la huruma wanakijiji hicho ili waonje matunda ya uhuru.
Akizungumza na mwandishi, diwani huyo alisema changamoto hiyo ni kubwa na ya siku nyingi huku akisisitiza kwamba ataacha wadhifa huo kama Serikali haitafikisha huduma ya maji safi na salama katika kijiji hicho.
"Sitaona sababu ya kuendelea na nafasi hii kama Serikali haitaona umuhimu wa kuleta maji katika kijiji hiki kwani wananchi wangu wanatabika ,ndoa zinavunjika, wajawazito wanataabika kusaka maji, "alisema.
No comments:
Post a Comment