“Mbali
na kukuza uchumi na kuongeza fursa za ajira nchini, viwanda hivi ndivyo
vitakavyotufanya tununue bidhaa kwa bei nafuu tofauti na ilivyo sasa
kwa kuwa vitu vingi vinaagizwa kutoka nje ya nchi,” alisema.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumatano Julai 13, 2016) wakati akikagua
ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Goodwill Tanzania
Ceramic katika kijiji cha Mkiu wilayani Mkuranga, Pwani.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Bw. Frank Yang alisema
jumla ya ajira 4,500 zinatarajiwa kutolewa kiwandani hapo mara ujenzi
utakapokamilika.
Akifafanua
kuhusu ajira hizo Bw. Yang alisema ajira 1,500 zitakuwa rasmi na zisizo
rasmi zitakuwa 3,000 huku wakazi wanaoishi katika maeneo yanayozunguka
kiwanda hicho wanatarajiwa kupewa kipaumbele. Mkurugenzi huyo alisema
ujenzi wa kiwanda hicho utagharimu dola milioni 100 na utafanyika kwa
awamu mbili. Awamu ya kwanza inatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu.
“Ujenzi
wa kiwanda hiki utainua ukuaji wa uchumi nchini Tanzania kwani
utakapokamilika Serikali itakusanya sh. bilioni 30 kwa mwaka ikiwa ni
mapato ya kodi,” alisema.
Naye
Balozi wa China nchini Tanzania Dk.Lu Youqing aliipongeza Serikali ya
Tanzania kwa kuchagua sekta ya viwanda kuwa ndiyo kipaumbele chake
katika kukuza uchumi. Alisema mbali ya ujenzi wa kiwanda cha vigae
katika eneo hilo pia wawekezaji hao kutoka nchini China wanatarajia
kujenga viwanda vya mbolea, karatasi na glasi (bilauli).
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu alipokea msaada wa madawati 500 yenye
thamani ya sh milioni 40 ambayo yalitolewa na Balozi wa China nchini Dk.
Lu kwa kushirikiano na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Goodwill
Tanzania Ceramic Bw. Yang.
No comments:
Post a Comment