Hata hivyo uwezo binafsi wa mchezaji husika walau unaweza kupandisha thamani yake katika soko la usajili ama kushusha kabisa thamani yake.
Wafuatao ni wachezaji ambao kupitia michuano ya Euro mwaka huu thamani yao inaweza kuwa imepeanda na baadhi yao kushuka.
Wachezaji ambao thamani yao imepanda
Moussa Sissoko
Sidhani kama kuna yeyote aliyeifuatilia kwa uzuri michuano ya Euro kama atabisha juu ya hili. Sissoko amekuwa na kiwango cha hali ya juu katika michuano hii na naamini hata timu yake ya Newcastle itashangaa, kwamba uwezo wa mchezaji wao huyu ulijificha sehemu gani kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Kwa namna moja ama nyingine anaamini Sissoko hatabaki Ligi daraja la Kwanza England ambapo timu yake itakuwa ikishiriki baada ya kushuka daraja msimu uliopita.
Joao Mario
Mreno huyu ama hakika amekuwa kwenye kiwango bora kabisa kwenye michuano ya Euro mwaka huu. Joa Mario ambaye kwa sasa anakipiga kunako klabu ya Sporting Clube de Portugal (Sporting Lisbon) ya nchini Ureno.
Ivan Perisic
Licha ya timu yake ya Croatia kutolewa katika hatua ya 16 bora na Ureno, lakini hakuna shaka kwamba uwezo wa Perisic ulikuwa ni wa hali ya juu kabisa. Alicheza vyema kuanzia mwanzo wa mashindano mpaka pale waliotolewa.
Alifunga goli muhimu la ushindi kwenye mchezo dhidi ya Uhispania ambapo Croatia walishinda magoli 2-1 na kuongoza kundi. Kwa sasa anakipiga kunako klabu ya Inter Milan lakini muda wowote anaweza kuondoka kuelekea kwenye vilabu vyenye hadhi zaidi.
Robbie Brady
Kabla ya Michuano ya Euro mwaka huu kuanza, Brady alitoka kupata machungu baada ya timu yake ya Norwich City kushuka daraja. Alifunga goli muhimu la ushindi dhidi ya Itlay katika hatua ya makundi na goli la penati dhidi ya Ufaransa. Amekuwa akihusishwa kwa karibu kutakiwa na klabu ya Leicester City na pengine kabla ya dirisha la usajili kufungwa rasmi anaweza kuwa amekamilisha dili hilo. Ni mchezaji anayesifika kwa upigaji mzuri wa mipira ya adhabu pamoja na kona.
Hal Robson-Kanu
Thamani yake ilikuwa ya chini sana kabla ya Michuano ya Euro mwaka huu kutokana na kuwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na klabu yake. Lakini uwezo wake kwenye timu ya taifa ya Wales umewashtua wengi. Goli lake muhimu dhidi ya Ubelgiji ni alama tosha ya ubora wake.
Arda Turan
Kabla ya Michuano ya Euro hakuwa kwenye kiwango bora kwenye klabu yake ya Barcelona. Michuano ya Euro ndiyo imezidi kuporomosha thamani yake kabisa. Ndiyo nahodha wa Uturuki lakini alishuhudia timu yake ikipoteza mechi mbili na kuibuka kwenye mchezo wa mwisho na kushinda. Baadaye aliomba radhi kwa mashabiki wao kwa kiwangokibovu cha timu yao. Kwa sasa Arda hawezi kutakiwa na klabu yoyote kubwa duniani kutokana na namna alivyoonesha kiwango chake katika siku za hivi karibuni.
Kama una kumbukumbu nzuri, huyu ndiyo mchezaji aliyefunga goli la ushindi katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia mwaka juzi dhidi ya Argentina. Kwenye klabu yake ya Bayern alikuwa hapewi nafasi kubwa katika msimu uliomalizika, na mbaya zaidi kwenye Michuano ya Euro ndipo alizikwa kabisa. Kocha wake alipenda kumtumia Mario Gomez kutokana na kuamua kutotumia tena mfumo uliokuwa ukimpa nafasi.
Wayne Rooney
Kocha wake wa sasa kunako klabu ya Manchester United Jose Mourinho amesema hatamtumia katika nafasi ya kiungo badala yake atampa nafasi ya ushambuliaji.
Adil Rami
Alianza vyema kwa kupewa nafasi ya kucheza kwenye Michuano ya Euro akiwa na timu yake ya Ufaransa. Baadaye alipata adhabu iliyomweka nje na na nafasi yake kuchukuliwa na Samuel Umtiti. Umtiti alikaba kabisa nafasi ya Rami na kuondoa nafasi yake ya kutazamwa na vilabu vikubwa. Kwa sasa anakipiga na Sevilla na pengine ataendelea kubaki pale kutokana na kutokuwa na vilabu vyovyote kutajwa kumnyemelea.
No comments:
Post a Comment