Mgombea urais wa chama cha
Republican nchini Marekani Donald Trump amemchagua Mike Pence kuwa
mgombea mwenza, taarifa katika vyombo vya habari Marekani zinasema.
Maafisa
wa kampeni wa Bw Trump walipanga atangaze uamuzi wake Ijumaa, lakini
hafla hiyo ikaahirishwa kutokana na shambulio la kigaidi lililotokea
Nice, Ufaransa.Duru za karibu zimeambia shirika la habari la ABC News kwamba Bw Pence amekubali kuwa mgombea mwenza.
Hata hivyo, Bw Trump aliambia Fox News Alhamisi jioni kwamba: “Bado sijafanya uamuzi wangu wa mwisho, uamuzi wa mwisho.”
- US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama
Wagombea wengine ambao walipigiwa upatu kuchaguliwa na Bw Trump kuwa mgombea mwenza ni Spika wa Bunge Newt Gingrich na Gavana wa New Jersey Chris Christie.
Bw Pence ni gavana wa Indiana na mwanachama wa vuguvugu la siasa za mrengo wa kulia la Tea Party.
Akiteuliwa, basi Bw Pence atakuwa makamu wa rais wa Bw Trump iwapo atafanikiwa kumshinda mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton kwenye uchaguzi mkuu Novemba
No comments:
Post a Comment