Zaidi ya watu 80 wameripotiwa kuuawa katika shambulio lililotokea katika mji wa Nice kusini mwa Ufaransa.
Lori
lililokuwa likienda mwendo kasi lilijiingiza katika mkusanyiko wa watu
waliokuwa wakiangalia maonesho ya fataki kuadhimisha siku ya kitaifa ya
Bastille, ambayo huja na shamra shamra kila mwaka.Mwendesha mashtaka katika mji wa Nice, Jean- Michel Pretre amesema lori hilo liliendelea kutembea kilo mita mbili kabla ya polisi kumpiga risasi dereva.
- Kwa Picha: Shambulio la Nice, Ufaransa
- Hollande: Hatutabadili msimamo kuhusu ugaidi
Waakazi wa mji huo wa Nice wameshauriwa kutulia majumbani.
Rais Francois Hollande amerudi mjini Paris kwa ajili ya kufanya kikao cha dharura.
Hali ya tahadhari iliyowekwa toka kutokea kwa shambulio lililofanywa na Islamic State mjini Paris, bado iko palepale nchini Ufaransa.
No comments:
Post a Comment